Alhamisi hii malkia wa filamu nchini Wema Sepetu ameachiwa kwa dhamana
ya shilingi milioni tano baada ya kupandishwa kizimbani kwenye mahamaka
ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu
yanayomkabili.Wakati huo huo mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji na askofu Josephat Gwajima wamewasili katika kituo cha kati cha polisi kwa ajili ya kutii agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paulo Makonda ambapo majina yao yalitajwa Jumatano hii kuwa miongoni mwa majina 65 katika orodha ya watu wanatuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment