• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 6 March 2017

    Baraza la Madiwani Temeke lapitisha bajeti yake, Meya anena haya

    Baraza la Halmashauri ya wilaya yaTemeke limepitisha bajeti ya mwaka 2017-2018, yenye vipaumbele kadha wa kadha ikiwemo suala la Elimu, Miundombinu na huduma za afya, huku ikitatarajiwa kukusanywa bilioni 32.8 itakayo tokana na mapato ya ndani.
    Akitoa majumuhisho ya bajeti hiyo Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Abdallah Chaurembo amesisitiza kuwa itakuwa vizuri kama watendaji wakasimamia majukumu yao kwenye kuboresha elimu na kumuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nasib Mbaga kuzitafutia ufumbuzi shule mbili zilizopo eneo la uwekezaji kurasini aidha zitafutiwe muwekezaji kwa kila shule shilingi bilioni 5, pesa ambazo kwa ujumla wake ni bilioni 10 zinaweza zikatumika kutengeneza madawati takribani 500 au kujenga shule mbili moja Mwagala na Nyingine Temeke, au zinaweza kutumika kwenye uboreshaji wa masuala mengine ya kielimu.
    Pia Mstahiki Meya Chaurembo amesema katika kulinda falagha ya mtoto wa kike ni vyema kukawepo chumba maalum kwa kila shule kwa ajili ya stara ya mtoto wa kike, huku Katika suala la kiafya ameeleza kuwa Zahanati ya Charambe na Kijichi huenda ikakamilika mwezi wa saba lakini changamoto iliyopo kwa wakazi wa maeneo hayo ni umbali wa zahanati hizo kilomita moja kwa kila moja hivyo ni vyema Mkurugenzi na watendaji husika wakaboresha miundombinu itakayo pelekea wepesi wa kufika kwenye zahanati hizo.
    Pia ameiagiza ofisi ya Mkurugenzi kununua pump itakayo kuwa ya Halmashauri kwa ajili ya kusaidia maeneo korofi kipindi hiki cha masika, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nasib Mbaga amemhakikishia mstahiki Meya kuwa watanunua Pump hivi karibuni na kwayale maeneo korofi kabisa watamtafuta muwekezaji ili wananchi wa maeneo hayo walipwe pesa na wahame ili kunusuru maisha yao na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu, pia kuepuka mafuriko

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI