Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka wabunge, na madiwani kuiga mfano wa Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Hassan Zungu, kwa kuonesha waliyoyafanya kwa kipindi cha muda fulani.
DAS Mpogolo ameyasema hayo baada ya Mbunge Zungu kueleza aliyoyafanya kwa kipindi cha mwaka mmoja 2015-2016 na kuikabidhi ilani hiyo kwa Katibu Tawala na wananchi na baadhi ya wanachama.
DAS Mpogolo amesema alichokifanya mbunge Zungu ni cha kuigwa mfano kwani kinawasaidia wao kama serikali kujua wapi walikosea ili warekebishe au kuongeza nguvu, na maendeleo kupatikana.
Huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo kuna wasaidia wananchi kumuamini kiongozi wao na hatimaye kuitumia fursa yao ya kikatiba kwa kumchagua kiongozi anaefaa.
No comments:
Post a Comment