GSM wameamua kuwaunganisha Watanzania kwa kuwafungulia duka Mlimani City lengo likiwa kuwarahisishia upatikanaji wa bidhaa kwa karibu kabisa.
Cortefiel ni duka jipya ambalo limefunguliwa leo, linabidhaa kwa bei rahisi ambapo hata Mtanzania wa hali ya chini anaweza kununua bidhaa zao.
Mohamedi Saad ni 'brand manager' wa GSM Mall amewaomba wananchi wote wasiyaogope maduka yao kwani kuna bidhaa ambazo wanauwezo wa kuzinunua, bidhaa ambazo wanazinunua kariako ikiwa GSM wameziboresha zaidi. Bidhaa zinaanzia elfu 10 na kuendelea.
Aidha afisa masoko wa GSM amesisitiza kuwa duka hili limetoka Madrid Hispania kuna nguo kila aina mashati pamoja na fulana, huku kukiwa na viatu vyenye hadhi kubwa kwa bei nafuu.
No comments:
Post a Comment