Akizungumza Leo katika hafla fupi ya kukabadhi vifaa vya
shule Kwa wanafunzi wa sekondary ya mugambe, meneja masoko wa kampuni ya
simu ya itel Tanzania Saiphoni Asajile amesema kuwa Leo kampuni yao
ilikuwa inatoa vifaa vya shule hasa kwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu.
Aidha amesema kuwa wametoa mabegi 100 na karamu na hii ikiwa ni mwendelezo wa kuwa wanatoa vifaa kwa wanafunzi kwa kila mwezi.
Kwa upande wake Hamadi Mongomongo ambaye ni mwanafunzi wa
kidato cha pili katika shule za sekondary Mugabe amesema ni vema kwa
watu na makampuni binafsi kujitokeza kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji
maalumu ili kuwezesha kupata vifaa zaidi vya shule.
No comments:
Post a Comment