Uamuzi huo umetolewa Alhamisi hii mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela. Peter aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi.
Mbunge Lijualikali na Dereva wake, John Kibasa walihukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini kwa kosa la kufanya vurugu na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wakati wa kipindi cha uchaguzi mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment