Klabu
ya Dar Jogging imeandaa mbio za pole zitakazofanyika siku ya jumapili
ya tarehe 26. Machi, 2017. Mbio hizo zitaanzia uwanja wa Taifa kuelekea
Temeke Mwisho, Sudan, majaribio hadi uwanja wa Mwembe Yanga. Mbio hizo
zitaongozwa na Mshahiki Meya wa Temeke ndugu Abdallah Chaurembo
akiambatana na Mbunge wa Temeke Abdala Mtolea, baadhi ya madiwani kama
Diwani Benjamin Ndalichako wa Kata ya Chang’ombe, na wenyeviti wa
serikali za mitaa kama Mwenyekiti wa Serikali ya mitaa ya Chang’ombe
Ali Majata.
Bonanza
hili la jumapili linafanyika chini ya mwavuli wa Umoja wa Vilabu vya
jogging vya Upatu kwa kifupi UVIJO. Vilabu vilivyoko chini ya uvijo ni
pamoja na Dar Jogging, Dovya jogging, Temeke Family, Tupo Jogging,
vilivyoko katika wilaya ya Temeke. Vilabu vya uvijo vinavyotoka
Kinondoni ni pamoja na Barafu Jogging, Mzimuni Jogging, na Tunajenga
Jogging. Madhumuini ya vilabu vya Uvijo ni kufanya mazoezi pamoja kila
mwezi mara moja huku wakichangiana pesa zinazopokelewa na klabu moja
kila mwezi. Mtindo huu ulioanzishwa na vilabu hivi ni kama vile mtindo
ambao watu wengine wanafanya katika kuchangiana pesa maarufu kwa jina la
upatu, lakini vilabu hivi vinajikita zaidi kusaidiana kiuchumi na
kupeana mawazo ya nini cha kufanya hasa uendeshaji wa vilabu kiuchumi.
Vilabu
vingine vitakavyokuwepo katika mbio hizo ni pamoja na vilabu
vinavyounda Uvijo ni pamoja na Ferry Jogging, Haipotei Jogging,
Solidarity Jogging, Faita Jogging, Zebra Jogging, Soko Mjinga Jogging,
Mtoni Jogging, Mtongani Jogging, Kongowe Jogging, Serengeti Jogging,
Yombo City Jogging, New Heroes, Msakala Jogging, Na Buza Joggging.
Wengine
ni Waasisi Jogging, Kata 14 Jogging, Capela Bay Jogging, Mzalendo
Jogging, Washikaji/Kiujamaa Jogging, Denish Jogging, Afya na Uchumi
Jogging, Darajani Jogging, Matosa Jogging, Ukonga Jogging, Hananasifu
Jogging, Luwanga Jogging, Luwanga Jogging, Team Pamoja Jogging, Pamoja
Zaidi Jogging, Class Jogging, TEmeke Jogging, East West Jogging, Amani
Jogging, Mshikamano Jogging, Ukwamani Jogging, Ambushez Joigging na
Fanja Jogging.
Hatua
hii ya kufanya mazoezi ya kivikundi ni hatua mojawapo ya kuunga mkono
agizo la Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia
Suluh Hasan tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders.
Mwenyekiti wa Klabu ya Dar Jogging ameomba vikundi vingine na wananchi
kiujumla kuja kujumuika na Dar Jogging katika Bonzanza hili. Ndani ya
makundi haya kuna wanamichezo mbalimbali wapo kutoka michezo mingine
ikiwemo kuogelea, mpira wa miguu, netiboli, wavu, riadha na ngumi.
Tunawaomba watu wote waje kukimbia na sisi na wala hauhitajiki kulipa
kitu chochote.
Mwenyekiti
Namkoveka aliongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja
na kupata kibali kutoka kwa afisa utamaduni na michezo na wenzetu wa
Radio Times watajumuika nasi katika mbio hizo zitakazoishia Mwembeyanga.
Baada ya mbio hizo kufanyika mechi ya mpira wa miguu kati ya Times Fm
Radio pamoja na Dar Jogging mechi ambayo itafanyika katika uwanja huo
huo wa Mwembeyanga.
Ramadhan Namkoveka
Mwenyekiti
Dar Jogging and Sport Club
No comments:
Post a Comment