DC Mjema ameyasema hayo wakati wa kufungua semina iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa lengo la kutoa elimu juu ya masuala ya gesi nchini, ambapo DC Mjema amewasihi viongozi wa dini na madiwani kupitia semina hiyo ya siku moja waende wakawe mabalozi wema kwa wananchi na kuwaelekeza umuhimu wa kulinda miundombinu ya gesi na kutofanyabiashara za chakula maeneo hayo.
DC Mjema amefafanua kuwa umuhimu wa kufanya hivyo ni kuepuka mlipuko utakao tokana na mabomba ya gesi kuharibika kwa joto na hatima yake kupasuka na kupelekea mlipuko utakao teketeza maisha ya watu, hivyo ulinzi wa mabomba ya gesi ni muhimu sana kwa mustakabali wa maisha.
Pia DC Mjema ameeleza kuwa upatikanaji wa gesi nafuu kwa wananchi wote utapelekea kupungua kwa ukataji miti kwani matumizi ya mkaa yatapungua, mvua zitanyesha na hali ya hewa itakuwa nzuri tofauti na sasa.
No comments:
Post a Comment