• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 28 March 2017

    Mtanzania alie vunja record kupanda mlima kilimanjaro amvaa waziri wa habari sanaa na michezo



    Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada
    ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza
    kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka.
    Gaudence Lekule akipanda mlima Kilimanjaro huku akikimbia wakati akiweka
    rekodi baada ya kutumia muda wa saa 8:36 mapema mwaka huu.
    Lekule akifurahia mara baada ya kufanikiwa kuweka ekodi ya kutumia muda wa saa 8:36 kupanda Mlima Kilimajaro na kushuka.

    Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

    MTANZANIA ,Gaudence Lekule (31) anayeshiriki michezo ya kupanda milima
    kwa kasi (Mountain Run) amemuomba Waziri mpya wa Habari,Utamaduni Sanaa na
    Michezo ,Dkt Harison Mwakyembe kutupia jicho michezo mingine kwani ina nafasi
    kubwa ya kutangaza na kuletea sifa taifa.
    Lekule anayeshikilia rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza Duniani kupanda
    kwa muda mfupi katika Mlima Kilimanjaro akitumia muda wa jumla wa saa 8:36
    alitoa wito pia kwa kampuni,taasisi binafsi na za serikali kujitokeza kudhamini
    wanamichezo kutokana na eneo hilo upo uwezekano wa kujitangaza zaidi kidunia.
    Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum,Gaudence alisema kwa
    sasa yupo katika maandalizi ya kuweka rekodi mpya katika milima mirefu na
    maarufu  Duniani kwa kufanya mazoezi ya awali hapa nchini na baadae nje ya
    nchi.
    “ Nashukuru kuitangaza Tanzania kidunia na tayari nimepata  mialiko
    mingi ya kwenda nje kushiriki mashindano ya Mountain Run ,Lengo langu  ni
    kuweka rekodi katika milima mirefu duniani hivyo bado naendelea na mazoezi na
    nitaendelea kufanya mazoezi hapa kwetu na badaae nje ya Tanzania”alisema
    Gaudence .
    Alisema hadi sasa rekodi ya Dunia inashikiliwa na raia wa nchi ya
    Ecuador, Karl Egloff aliyetumia muda wa saa 6:53 kupanda na kushuka Mlima
    Kilimanjaro ,rekodi aliyoweka mwaka 2014 akivunja rekodi ya  Kilians
    Jornet  raia wa Hispania aliyetumia muda wa saa 7:20 kupanda na kushuka
    mlima Kilimanjaro mwaka 2010.
    Lekule alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni mabadiliko hali ya hewa
    inayochangia kushindwa kufanya mazoezi na upatikanaji wa mahitaji kama chakula
    pamoja na mavazi kwa ajili ya mchezo huo unafanyika kuanzia urefu wa mita 3500
    hadi 5800.
    Akizungumzia kilichomsukuma kushiriki mcezo mchezo huo,Lekule ,mkazi wa
    kiraracha Marangu wilaya ya Moshi alisema raia wa kigeni wamekuwa wakishiriki
    katika michezo ya aina hiyo kwa ajili ya kuweka rekodi hivyo akaona ni wakati
    wa waafrika pia kushiriki katika uwekaji wa rekodi Duniani.
     Alisema raia wa Ecuador ,anayeshikilia rekodi ya dunia aliposikia
    ameweka rekodi akiwa ni mwafrika na Mtanzania wa Kwanza alituma salamu za
    pongezi huku akimtaka kwenda kwenye milima iliyopo nchi za nje kutafuta rekodi
    nyinine.
    “ Egloff alifurahi sana na kunipa moyo na kunitaka nikatafute
    rekodi nje ya Afrika kwa sababu nina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri Ulaya
    na kuipa sifa Tanzania,ni ngumu sana mtu kukimbia kwenye urefu kama uliopo
    Mlima Kilimanjaro na katika maisha inahitaji moyo sana.”alisema Lekule.
    Rekodi za kidunia.
    Mara ya kwanza  rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kasi kwa
    Afrika ilikua inashikiliwa na Saimon Mtui akitumia muda wa saa 9 : 20 mwaka
    2006, baadae raia wa Hspania  Kilians Jornet  alitumia muda
    wa  saa 7:20  mwaka  2010.
    Mwaka 2014 ndipo Karl Egloff   raia wa Ecuador anayeshikilia
    rekodi ya Dunia hadi sasa alitumia muda wa  saa 6 :53 mwaka   2014
    na sasa  Mtanzania  Gaudence Lekule  ameweka rekodi ya kuwa
    Muafrika na Mtanzania wa Kwanza akitumia muda wa saa 8:36

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI