• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 8 March 2017

    Trump asaini sheria mpya ya kuzuia wahamiaji kuingia Marekani

    Rais wa marekani, Donald Trump amesaini sheria mpya ambalo litawazuia wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi sita zenye Imani kali ya Kiislamu kutokuingia Marekani.
    Nchi ambazo Trump amezizuia ni Iran, Somalia, Sudan, Yemen, Syria na Libya huku Iraq ikitolewa katika listi iliyokuwepo awali kwa sababu ambazo zilitajwa awali Iraq kuwa moja ya nchi ambazo zinaongoza mashambulizi ya kupambana na makundi ya kigaidi.
    Akizungumza baada ya kusaini sheria hilo, Rais Trump amesema lengo sio kuwazuia Waislamu kuingia bali ni kuimarisha usalama wa Marekani ili kuzuia hatari ambayo inaweza kujitokeza kama wakiruhusiwa.
    “Hatuwahitaji hapa,” alisema Trump kuhusu magaidi; “Tunataka kuhakikisha kuwa kila anayekuwa nchini kwetu anaisapoti nchi yetu na kuwapenda watu wetu.”
    Aidha serikali ya Marekani imesema wananchi wan chi ambazo wamezuiliwa hawataweza kuingia Marekani na utaratibu wa kutoa visa kwa watu hao utazuiliwa kwa siku 90 kisha wataangalia utaratibu gani utumike.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI