Meneja Mradi wa Kampuni ya
Songoro Marine Transport inayojenga Kiuvko cha MV. Kazi, Bw. Major
Songoro, akitoa ufafanuzi wa mashine kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokagua Kivuko hicho jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akiangalia moja ya vifaa
vilivyoko kwenye chumba cha kuendeshea kivuko katika kivuko cha MV. Kazi
kinachojengwa jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kitakabidhiwa tarehe
15 Mwezi huu. Wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme nchini (TEMESA), Dkt. Musa Mgwatu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akifafanua jambo kwa Uongozi
wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mara baada ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi ambacho kinatengenezwa
jijini Dar es salaam na Kampuni ya Songoro Marine Transport.
Mafundi wa Kampuni ya Songoro
Marine Transport, wakiendelea na kazi ya kufunga mashine katika Kivuko
cha MV Kazi. Kivuko hicho kitakamilika na kukabidhiwa wiki ijayo na kina
uwezo wakubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Kivuko cha MV. Kazi kikiwa katika
hatua za mwisho za ujenzi wake.Kiuvko hicho kitakamilika na kuanza
tarehe 15 mwezi huu na kina uwezo wakubeba abiria 800 na magari 22 kwa
wakati mmoja.
…………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka uongozi wa Wakala wa Ufundi
na Umeme nchini (TEMESA) kushiriki kikamilifu shughuli za matengenezo ya
vivuko ili kupata ujuzi wa ufungaji wa mifumo kutoka Kampuni
zinazotengeneza vivuko vya Serikali.
Akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuvko kipya cha MV
Kazi, Bandarini jijini Dar es Salaam, Waziri Prof. Mbarawa amesema
kuwa kupitia mafunzo hayo Serikali itaweza kuokoa fedha nyingi ambazo
kwa sasa inatumia kulipa kampuni binafsi zinazojenga na kukarabati
vivuko
“Hakikisheni mnapata ujuzi kama
walionao hawa, hatutaki kutumia fedha za Serikali kwa ajili ya
kukarabati au kutengeneza vivuko wakati nyinyi TEMESA mpo”, amesema
Waziri Prof. Mbarawa
Pamoja na ujenzi wa kivuko hicho
Waziri Mbarawa amewataka Temesa kuhakikisha wanasimamia na kukitunza
kivuko hicho ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.
Aidha, Profesa Mbarawa ameuagiza
Wakala huo kuhakikisha wanakamilisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa
njia ya kielektroniki ili ili kudhibiti mianya ya rushwa.
Kuhusu huduma za kivuko mkoani
Lindi Serikali imesema itahakikisha inapelekea huduma haraka
iwezekanavyo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mkoa huo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
Wakala huo Dkt. Musa Mgwatu, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Songoro
Marine Transport kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili
kukamilisha kivuko hicho kwa muda uliopangwa.
Dkt. Mgwatu amefafanua kuwa
kukamilika kwa kivuko hicho kutarahisisha usafiri kwa wakazi wa
Kigamboni na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam ambao wamekuwa
wakitumia huduma hiyo katka shughuli zao za kila siku.
Nae, Meneja Mradi wa Kampuni ya
Songoro Marine Transport, Bw. Major Songoro amemhakikishia Waziri
Mbarawa kumaliza kivuko hicho kwa wakati ambapo amesema ifikapo tarehe
15 mwezi huu kivuko hicho kitakabidhiwa kwa Serikali.
Bw. Songoro amefafanua kuwa kwa
sasa mafundi wanamalizia kazi ndogo ndogo zilizobaki ikiwa ni pamoja na
kumalizia ufungaji wa injini.
Kivuko kipya cha MV Kazi
kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni Saba na kina uwezo wa kubeba
abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja
No comments:
Post a Comment