Suruali za jeans ndizo suruali pekee ambazo huvaliwa zaidi na kupendwa na watu wengi duniani.
Tukizungumzia jeans kwa kipindi hiki basi usisahau kutaja Ripped
Jeans(jeans za kuchanwa chanwa), ambazo zinazidi kuvaliwa kila kukicha
na watu. Muonekano wa suruali hii unaweza ukakufanya ustaajabu ikiwa
bado haijavaliwa na mtu.
Vjiana ndio asilimia kubwa ya wavaaji wa suruali hizi za kuchanwa
chanwa. Mwaka 2011 suruali zilianza kuingia madukani na kuvaliwa. Ingawa
ilikua kazi kuwashawishi watu kuvaa jeans hizo, ongezeko la wavaaji
linazidi kuongezeka.
Ripped jeans ama jeans za kuchanwa chanwa inaweza kuvaliwa sehemu
yoyote , na ni vizuri ikivaliwa sehemu za burudani kama matamsha ya
kimuziki.
Hata hivyo, suruali hizii hazifai ofisni na mahala pa kazi.
Zipo Ripped jeans tofauti tofauti yani za watu wenye miili mikubwa( wanene) na wenye miili membamba kwa watu wa jinsia zote.
No comments:
Post a Comment