Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Serikali imewasahuri wananchi
wote wanaofaidika na Mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF) nchini
kuzitumia vizuri ruzuku wanazozipata kwa kuendelea kujishughulisha na
shughuli za kiuchumi katika maeneo yao.
Akijibu swali la Mbunge wa Mtabwe
Mhe. Khalifa Mohamed Issa lililouliza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) upo katika Awamu ya Tatu ya Utekelezaji wa Mpango wa kunusuru
Kaya Maskini nini kimefanyika ili ruzuku ziweze kumudu mahitaji ya
chakula, Elimu, Afya na lishe Bora kwa watoto.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema kuwa Serikali
inaendelea kutoa ruzuku wa Kaya Maskini ila inasahuri pia wananchi
waendelee kujishughulisha na kazi nyingine za kuongeza kipato na
isitegemee ruzuku pekee.
“Niwaombe wananchi wanaopata
ruzuku kutoka mpango wa TASAF wajishughulishe pia na shughuli nyingine
za kiuchumi na kutotegemea ruzuku pekee” Alisistiza Mhe. Angella.
Ameongeza kuwa ruzuku
zinazotolewa ni kichocheo cha kuifanya kaya iweze kujikimu hasa katika
kupata mahitaji muhimu huku ikiendelea kujiimarisha kiuchumi kwa kuweka
akiba na kutekeleza miradi ya ujasiriamali ili iweze kusimama yenyewe na
kujitegemea baada ya kutoka katika umaskini uliokithiri.
Mhe. Angella Kairuki ameeleza
kuwa vigezo vya kupata kaya maskini ni wa uwazi na huanishwa na Jamii
katika mkutano wa hadhara unaoendeshwa na wawezeshaji kutoka Halmashauri
za Wilaya na kusimamiwa na Viongozi wa Vijiji, Mitaa na Shehia.
Aidha uzoefu uliopatikana
umeonesha kwamba kwa kiwango cha ruzuku kinachotolewa kwa wananchi
wanaofaidika na Mpango huo kimewawezesha kuboresha maisha yao kwa
kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ufugaji,ujasiriamali na
ujenzi wa nyumba bora, hivyo viwango hivyo sio vidogo kama wengi
wanavyodhani
No comments:
Post a Comment