Katika kikao kilichofanyika jana mjini Zanzibar, kiliazimia kuwateua Profesa Abdalla Safari, Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan, Lawrence Masha na Pamela Massay.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene imesema wateule hao watakamilisha hatua zingine za uteuzi kwa mujibu wa utaratibu, Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki.
Soma majina yao hapa:
Kwa upande wa CCM, wabunge wapya wa EALA walioshinda ni Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe na Adam Kimbisa na kutoka CUF iliyokuwa na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo.
No comments:
Post a Comment