Msanii anaebamba na ngoma ya Dozee kwa sasa na kutokea label ya PKP, Nedy Muzik amewachana wasanii kutokea kisiwani Zanzibar kuwa waache kulalamika.
Nedy alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo-East Afrika Radio, kuwa wasanii wa zanzibar waache kulalamika kwa kukosa usimamizi kuwa ndio chanzo cha wao kushindwa kufanya muziki wa bongo flava.
“Siyo kwamba wadau wa muziki wa Zanzibar wameshindwa kuwekeza, lakini wanaogopa kutoa pesa pasipo kuwa na uhakika kama mahali anapowekeza patamletea manufaa kwake kwake na msanii huyo” alisema Nedy
Nedy pia aliwataka wasanii hao kutokea kisiwani huko ambako na yeye anatokea, kutotumia silaha ya dini kwani muziki ni sehemu ya ajira hivyo wanatakiwa kutenga muda wa kazi na muda wa ibada.
No comments:
Post a Comment