Mwenyekiti wa klabu ya Dar es
salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akizungumza na vyombo vya habari
leo jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100
tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya
michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa
kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa
Julai 08. Katikati ni Meneja Msaidizi wa klabu hiyo, Elizabeth Michael
na kushoto ni Mratibu wa Masoko na Matukio Levina George.
Meneja wa Mauzo wa Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana na udhamini wa mashindano
yatakayosindikiza maadhimisho ya miaka 100 ya klabu ya Dar es Salaam
Gymkhana tangu ilipoanzishwa mwaka 1916. Katika kuadhimisha siku hiyo ya
kihistoria, klabu imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali
kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine
mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai
08.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ndio mdhamini Mkuu wa mashindano
hayo. Wadhamini wengine wa mashindano hayo ni pamoja na Clouds Media
Group, Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance
brokers, Vodacom na Mwananchi Communications.Kushoto ni Mwenyekiti wa
klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta.
Mwenyekiti wa klabu ya Dar es
salaam Gymkhana, Walter Chipeta (katikati) akisikiliza maswali toka kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo
jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya
michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa
kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa
tarehe Julai 08. Kulia ni Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) Ndugu Itandula Gambalagi na Meneja Msaidizi wa klabu hiyo,
Elizabeth Michael (kushoto).
Mwenyekiti wa klabu ya Dar es
salaam Gymkhana, Walter Chipeta akisalimiana na Meneja wa Mauzo wa
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi wakati wa
mkutano wa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko
mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo
imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi,
Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa
kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.
…………………………………………………
Klabu ya Gymkhana Dar es salaam
inayojihusisha na michezo ya aina mbalimbali imejipanga kusherehekea
kutimiza miaka 100 kwa staili ya tofauti tangu kuanzishwa kwake mwaka
1916.
Katika kuadhimisha tukio hilo la
kihistoria, Klabu hiyo imeandaa idadi ya michezo mbalimbali
itakayosindikiza maadhimisho hayo ambapo michezo hiyo inatarajiwa kuanza
tarehe 03 Julai, 2017 na kuhitimishwa tarehe 08 Julai kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bw. Walter Chipeta.
Miongoni michezo iliyopangwa
kufanyika katika kuadhimisha miaka 100 ya klabu hayo ni pamoja na Gofu,
Tenisi, Skwashi, Soka, Kriketi, mchezo wa kuogelea na mingine mingi
ambayo kwa ujumla itawahusisha wanachama na wasio wanachama wa klabu
hiyo.
Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Klabu ya
Gymkhana, Walter Chipeta alisema, “Maadhimisho ya miaka 100 ni tukio la
kihistoria kwa ajili ya klabu yetu na tumejipanga kusheherekea shughuli
hii kupitia michezo mbalimbali ambayo itaanza rasmi tarehe 03 Julai na
kilele chake kuwa tarehe 8 Julai.”
Chipeta alisema klabu hiyo
inawakaribisha wanachama na wasio wanachama kutoka ndani na nje ya
Tanzania ili kushiriki kwenye maadhimisho hayo na kusisitiza kwamba
washiriki watafurahia na kuburudika.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao ndio wadhamini rasmi wa
maadhimisho ya miaka 100 ya Gymkhana Ndg. Itandula Gambalagi alisema,
“Tunajisikia fahari kuhusishwa na klabu kubwa kama hii na kwenye tukio
la kihistoria kama hili la kuikumbuka klabu hii kongwe. Aliongeza kuwa
tukio hilo litatoa fursa kwa NHC kujitangaza zaidi na kukutana na wateja
wake muhimu katika mazingira tulivu ya kijamii.”
Licha ya NHC kuwa wadhamini rasmi
wa shughuli hiyo, Klabu ya Gymkhana pia ilitoa shukrani kwa wadhamini
wengine wa mashindano hayo ambao ni pamoja na Clouds Media Group, Qatar
Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance brokers,
Vodacom na Mwananchi Communications.
Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana
ikiwa ni kituo au sehemu ya kukuza michezo, kwa miaka mingi imekuwa ni
chombo muhimu kinachowaunganisha watu kupitia michezo na shughuli
mbalimbali za kijamii.
Pia, imekuwa ikiendesha michezo ya
watoto na watu wenye ulemavu ambao pia wanapata fursa ya kushiriki
michezo kama tenisi na Skwashi.
Hii ni klabu ambayo inapokea watu
wote wanaopenda kuwa sehemu ya jumuiya ya wapenda michezo na kuwa sehemu
ya maadhimisho haya ya kihistoria ili kuendelea kukuza michezo
mbalimbali
No comments:
Post a Comment