Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina
mama wajawazito wakati na baada ya kujifungua vilivyotolewa na Shirika
la Red Crescent la Kuwait ambapo mabeseni 100 yenye vifaa hivyo kati ya
1000 yalikabidhiwa kwa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, Dar Es Salaam.
Balozi
wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akihutubia mbele ya Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa
zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati
kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo
zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na
Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye
vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho
kilipokea mabeseni 100.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa
zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati
kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo
zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na
Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye
vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho
kilipokea mabeseni 100,Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya mabeseni yenye vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu
Hassan pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakiangalia mbabeseni
yanya vifaa vya kusaidia wakina mama kujifungua yaliotolewa na Shirika
la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Bi.Arafa Nurdin wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya
hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa
vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Mbagala Rangi Dkt. Joseph Kiani wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya
hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa
vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na
Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000
yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya
Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na
kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimsalimia mtoto mwenye miezi miwili Jenifer Mathias, kulia ni
baba wa mtoto Bw. Mathias Miano mkazi wa Kingugi, Mbagala kabla uzinduzi
wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati
kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo
zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na
Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye
vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho
kilipokea mabeseni 100
Sehemu
ya wananchi wa Mbagala Kizuiani kwenye kituo cha Afya cha Mbagala Round
Table waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa zoezi la
kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua
vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya
mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar.
……………………………………………………..
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amezindua zoezi la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 200 yaliyotolewa
na Ubalozi wa Kuwait nchini kwa ajili ya wanawake wajawazito katika
hospitali ya Mbagala Zakiem na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table
katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Lengo la mpango huo ni kutoa mabeseni hayo zaidi ya 1,000 kwa
wanawake wajawazito wasio na uwezo kwa upande wa Tanzania Bara na
Zanzibar kama hatua ya kukabiliana na vifo vya watoto na wanawake
wajawazito nchini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa tiba hivyo,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan amesema kuwa mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika
kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito kwa kukosa vifaa
tiba kutokana na umaskini unaowakabili.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa maeneo
yaliyopatiwa mabeseni yenye vifaa tiba yahakikishe vifaa hivyo
vinatolewa kwa wanawake wajawazito ambao baadhi yao wanakata tamaa
kwenda kujifungulia kwenye hospitali au kwenye vituo vya afya kwa
kukosa vifaa hivyo kwa sababu ya umaskini.
Amesema mkakati uliopo wa Serikali ni kuhakikisha huduma za afya
nchini zinaendelea kuboreshwa hasa huduma ya mama na mtoto ambapo
kutokana na umuhimu wa sekta ya afya Serikali imetenga fedha za kutoka
katika bajeti ya mwaka 2017/2018.
Makamu wa Rais ameeleza kuwa mradi huo wa ugawaji wa mabeseni yenye
vifaa tiba katika mradi huo kuanzia sasa utasimamia na wake wa viongozi
wastaafu na wakiwemo wake wa mawaziri baada ya kuuzindua rasmi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia ameishukuru Serikali ya
Kuwait kwa msaada wake huo ambao amesema utakuwa ni chachu ya kupambana
na vifo vya watoto na wanawake wajawazito Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa upande wake, Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesema
Serikali ya Kuwait kupitia kwa Jumuiya ya Red Crescent ya nchini hiyo
itaendelea kusaidia vifaa tiba mbalimbali kwa upande wa Tanzania Bara na
Zanzibar ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu
na maeneo yao.
Balozi huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesisitiza kuwa
milango ya ubalozi wa Kuwait ipo wazi kwa Taasisi mbalimbali za
Kiserikali kupeleka maandiko mbalimbali kwa ajili ya kuomba kupatiwa
misaada lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma
za viwango vya juu katika sekta mbalimbali.
Amesema kwa sasa Serikali ya Kuwait ipo mbioni kutiliana saini ya
makubaliano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kufanya
ukarabati mkubwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo Unguja.
Ameeleza kuwa ukarabati huo utaiwezesha hospitali hiyo kuongeza utoaji wa huduma bora kwa wananchi wengi zaidi.
Halfa ya makabidhiano ya mabeseni 200 ya vifaa tiba katika hospitali
ya Mbagala Zakiem na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika
wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi
mbalimbali ikiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
..

No comments:
Post a Comment