Prof. Kabudi akiwa na bibi Zaman balsa ya kumaliza mazungumzo ya yaliyofanyika ofisini kwake mjini Dodoma
……………….
Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemkutana na Mwakilishi mkazi WA
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto duniani-UNICEF
bibi Maniza Zaman ofisini kwake mjini Dodoma.
Katika kikao hicho viongozi hao mbali na kufahamiana pia wamejadili namna ya kuboresha mahusiano baina ya Wizara na UNICEF .
Katika maongezi hayo
Bi. Zaman aliishukuru Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano inayowapa
UNICEF katika programu mbalimbali inazoshirikiana na Wizara.
UNICEF inatekeleza
kwa kushirikiana na Wizara katika maeneo ya usajili wa watoto chini ya
miaka mitano na kuwapa vyeti vya kuzaliwa, huduma ya msaada wa kisheria
na mkakati wa haki mtoto
No comments:
Post a Comment