• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 13 July 2017

    Cuf walia na chadema

    Siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kujitosa kwenye mgogoro wa Chama cha Wananchi CUF, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya ameibuka na kusema hawatazivumilia hujuma za chama hicho.
    Naibu katibu mkuu wa CUF Magdalena H. Sakaya akiongea na waandishi wa habari mapema jana makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam


    Akizungumza katika Ofisi za CUF Makao Makuu Buguruni, Sakaya amesema mara kadhaa wameripoti matamko ya viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiingilia mgogoro wa CUF.
    “Chadema wamekuwa na vikao kadhaa na mkakati wa kuhakikisha wanaifuta CUF upande wa Bara, miongoni kwa mipango hiyo ni kuvamia Ofisi pamoja na kuratibu na kukusanya vijana wa kihuni.” – Magdalena Sakaya.
    Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria mkutano huo mapema jana jijini Dar es salaam
    Aidha, Sakaya amesema kuwa CUF wanalichukilia jambo hilo kuwa ni kushindwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi kuiuza CUF kwa Chadema.
    “Tunawataka Watanzanua wafahamu kuwa CUF ni chama kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria na kina Katiba yake. Hivyo hatutotoa fursa ya kufanyiwa maamuzi nje ya vikao vya chama na tunatoa onyo kwa viongozi wa CHADEMA.” – Mgdalena Sakaya
    Baadhi ya wanachama wa CUF wakiimba nyimbo za kujigamba kuonyesha kutowaogopa CHADEMA

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI