Waziri
wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akizungumza
na Waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na maadhimisho ya siku ya
Idadi ya Watu duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo July,11. Kulia
yake ni Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Juma Hassan Reli.
Baadhi
ya wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na Waziri wa Fedha na
Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed hayupo pichani uliofanyika
wizarani kwake Mjini Zanzibar.
Mwandishi
wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza swali kwa
Waziri wa Fedha na Mipango juu ya siku ya Idadi ya Watu duniani katika
mkutano uliofanyika Wizarani kwake Vuga.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akitoa ufafanuzi wa maswali alioulizwa na wandishi wa habari.
Picha na Makame Mshenga.
Na Maelezo Zanzibar
Wakati
dunia inaungana kuadhimisha siku ya Idadi ya Watu duniani bado uzazi wa
Mpango unaonekana ni changamoto katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar.
Hali
hiyo hupelekea ongezeko la idadi ya watu lisiloendana na kasi ya ukuaji
wa uchumi na upatikanaji wa huduma za jamii katika maeneo mbalimbali
nchini.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dkt. Khalid Salum wakati akitoa taarifa yake kwa Vyombo vya
habari kuelekea maadhimisho hayo hapo kesho.
Amesema
ni vyema jamii kujenga mwamko juu ya umuhimu wa suala la uzazi wa
Mpango ili kujenga jamii bora, iliyoimara na chachu katika kuongeza kasi
ya maendeleo.
Dkt.
Khalid amesisitiza jamii kuendelea kutumia njia za asili za uzazi wa
mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama na kuhudhuria katika Vituo vya
afya kupata taaluma ya matumizi ya njia za kisasa pale inapohitajika.
Ameongeza
kuwa suala la uzazi wa Mpango limesisitizwa hata katika Vitabu vya Dini
ili kumpa nafasi Mama mzazi kurudisha afya na nguvu anazozitumia wakati
wa kubeba mimba na kujifungua.
No comments:
Post a Comment