MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,
amesema miongoni mwa Makampuni Binafsi yanayoisaidia Serikali kwa
kufanya kazi ya uuzaji na upimaji wa Viwanja vya Viwanda na Makazi, ni
Kampuni ya Property International pekee ambayo mpaka sasa kama mkuu wa
mkoa bado hajapata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu migogolo ya
ardhi.
Akizungumza
katika Kipindi cha Sema Kweli kinachorushwa kila Ijumaa na Kituo cha
Televisheni cha Channel Ten, alisema kuwa, amekuwa akipata malalamiko
kadhaa kutoka kwa wananchi juu ya migogolo hiyo inayotokana na kuuziwa
ama kupimiwa viwanja na makampuni ambayo hayajajitosheleza katika
kufanya kazi hiyo baada ya kuidhinishwa na Serikali.
Aidha
alisema kuwa kutokana na suala hilo kumekuwa na ugumu wa Serikali
kukusanya mapato ‘Kodi ya majengo’ kutokana na wananchi kujijengea
makazi holela bila kupata vibali vya ujenzi, baada ya kuuziana maeneo
kienyeji bila kupimwa na kupatiwa hati, jambo ambalo kwa sasa
linafanyiwa kazi kwa kasi na baadhi ya makampuni binafsi ikiwamo ya
Property International, yanayoshirikiana na Selikali katika kifanya kazi
hiyo.
Makonda
alimpongeza Waziri William Lukuvi, kwa kazi ngumu anayofanya ikiwa ni
pamoja na ya ulasimishaji wa makazi ili kwenda na viwango vinavyotakiwa
kwa ajili ya kuzitambua nyumba na kuzipa madaraja tofauti kurahisisha
upatikanaji wa kodi ya majengo, na mpangilio wa miji unaotakiwa huku
Serikali ikiendelea kuwakaribisha wapimaji biasfi ili kuendana na kasi.
”Wapimaji
binafsi watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa Watumishi na Vifaa
vya kisasa vinavyorahisisha upimaji wa haraka na kwa wakati, lakini
Manispaa zinatakiwa kuwapa ushirikiano makampuni hayo kwa kuwapa na
kuwatambua ili Serikali inapotoa Hati isitokee mgongano kutokana na
maeneo husika kupimwa na watu watatu tofauti”. alisema
Akiongelea
kuhusu Makampuni binafsi yanayotambulika na kuisaidia Serikali kufanya
kazi ya Upimaji, aliitaja Kampuni ya Property International, ambayo ina
jumla ya Viwanja 240 vya Viwanda huko eneo la Kigamboni jijini Dar es
Salaam, ambapo anayehitaji Heka hata 500 hadi 1000 anaweza kupata
ambavyo tayari vimepimwa na zaidi ya Viwanja 800 vya Makazi na Biashara
vilivyopimwa katika mradi huo.
Akizungumza
na Mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Property
International, Haleem Zahran , alisema kuwa Kampuni imefarijika sana
baada ya kusikia taarifa za serikali kutambua mchango na juhudi zinazofanywa na kampuni yake katika kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha suala la kupanga na kupima Viwanja katika maeneo mbalimbali ili wananchi kuweza kupata makazi yaliyo salama.
baada ya kusikia taarifa za serikali kutambua mchango na juhudi zinazofanywa na kampuni yake katika kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha suala la kupanga na kupima Viwanja katika maeneo mbalimbali ili wananchi kuweza kupata makazi yaliyo salama.
Hata hivyo alimpongeza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda
na Waziri Lukuvi kwa kazi kubwa wanavyofanya katika Sekta hiyo ili
kuendana na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo baada ya muda
kila mwananchi atakuwa akiishi katika eneo linalotambulika na kupunguza
migogolo ya ardhi.
‘’Kama
kampuni bado tuna mikakati mikubwa ya kuendelea kuongeza mashine za
kisasa za kurahisisha upimaji wa maeneo kwa haraka na uhakika”. Alisema Haleem
Aidha alisema kuwa Kampuni yake inaendelea na juhudi za kuiunga mkono Serikali na kwamba haitalewa sifa kwa kutambulika huko bali itaongeza jitihada na kupambana ili kuhakikisha inaisadia Serikali kupanga na kupima maeneo mbalimbali.
Aidha alisema kuwa Kampuni yake inaendelea na juhudi za kuiunga mkono Serikali na kwamba haitalewa sifa kwa kutambulika huko bali itaongeza jitihada na kupambana ili kuhakikisha inaisadia Serikali kupanga na kupima maeneo mbalimbali.

No comments:
Post a Comment