Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) Mhandisi
Joshua Mgeyekwa akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa
habari mapema hivi karibuni Ofisini kwake kuhusu mafanikio yatokanayo na
utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa Zigi. Filamu hiyo imeelezea namna
wanachi wanaozunguka maeneo ya mto Zigi uliopo Muheza Mkoani Tanga
wanavyoathiriwa na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Afisa Uhusiano wa Umma wa Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) Bi. Dorah
Killo akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Tanga Uwasa, Mhandisi Joshua Mgeyekwa (katikati) na waandishi wa habari
mapema hivi karibuni Ofisini kwake kuhusu mafanikio yatokanayo na
utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa Zigi. Filamu hiyo imeelezea namna
wanachi wanaozunguka maeneo ya to Zigi uliopo Muheza Mkoani Tanga
wanavyoathiriwa na uharibifu wa vyanzo vya maji. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Kampuni iliyotengeneza Filamu hiyo Bw. Humphrey Mgema .
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA)
wakifuatilia mkutano baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo
(hayupo pichani) na wandishi wa habari mapema hivi karibuni Ofisini
kwake kuhusu mafanikio yatokanayo na utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa
Zigi. Filamu hiyo imeelezea namna wananchi wanaozunguka maeneo ya mto
Zigi unaounganisha wilaya za Muheza, Mkinga na Tanga wanavyoathiriwa na
uharibifu wa vyanzo vya maji
Mtaalam wa Mazingira na Afisa
Ubora na Viwango Ramadhan Nyabuke akielezea jambo wakati wa mkutano
baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo (hayupo pichani) na
wandishi wa habari mapema hivi karibuni Ofisini kwake kuhusu mafanikio
yatokanayo na utafiti kupitia Filamu ya Mamba wa Zigi. Filamu hiyo
imeelezea namna wananchi wanaozunguka maeneo ya mto Zigi unaounganisha
wilaya za Muheza, Mkinga na Tanga wanavyoathiriwa na uharibifu wa vyanzo
vya maji.
……………………………………………………………………
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO-DAR ES SALAAM
TAARIFA
ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2004 inaonesha kuwa ifikapo mwaka 2025,
nchi za Bara la Afrika hususani zilizopo kusini ya jangwa la Sahara,
zitakumbwa na upungufu mkubwa wa maji kutokana na ongezeko la watu na
matumizi ya maji yasiyo endelevu.
Aidha
inakadiriwa kuwa upatikanaji wa maji kwa kila mtu kwa mwaka utapungua
toka mita za ujazo 2,300 za sasa hadi 1,500 ifikapo 2025 kutokana tatizo
la kuharibika na kupotea kwa vyanzo vya maji.
Pamoja
na umuhimu wa maji kueleweka na kila mwananchi, taarifa zinaonyesha
kuwa vyanzo vingi vya maji nchini vimeendelea kuharibika kwa kasi na
kusababisha maji kupungua katika mito na maziwa mengi.
Ili
kukabiliana na hali hiyo, Serikali inatekeleza Programu ya Maendeleo ya
Sekta ya Maji 2006-2025 inayolenga katika kuhimiza na kusisitiza usawa
na utashi katika utunzaji na usimamizi wa rasilimali za maji katika
maeneo ya mijini na Vjijini.
Kwa
hapa nchini, huduma ya usambazaji wa maji safi na salama na uondoaji wa
majitaka Mijini inatekelezwa na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa
Mazingira katika Miji Mikuu ya Mikoa, Wilaya, Miji Midogo.
Inaelezwa
kuwa wastani wa uzalishaji wa maji katika miji mikuu ya mikoa imepungua
kutoka lita milioni 470 kwa siku mwezi Machi 2016 hadi kufikia lita
milioni 400 kwa siku mwezi Machi, 2017 kutokana na kupungua kwa wingi wa
maji katika vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika
kukabiliana na changamoto hiyo, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) kwa kushrikiana na Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Tanga mwaka 2015 ilizindua Filamu ya utafiti ya Mamba wa Zigi iliyoelezea
kuhusu uharibifu wa mazingira katika milima ya usambara ambayo ndio
chanzo kikuu cha upatikanaji wa maji Jijini Tanga.
Akizungumza
hivi karibuni na Waandishi wa vyombo vya Habari Jijini humo, Mkurugenzi
Mtendaji wa TANGA UWASA, Mhandisi Joshua Mgeyekwa anasema kabla ya
uzinduzi wa filamu, mamlaka hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa
ya uharibifu wa mazingira katika mito midogo midogo inayounganisha Mto
Zigi na Bwawa la Mabayani na hivyo kutishia uendelevu wa huduma ya
kusambaza maji Jijini Tanga.
Anasema
utafiti wa filamu hiyo ulionyesha kuwa shughuli za kijamii na kiuchumi
zikiwemo kilimo, ukataji miti, uogeshaji mifugo, na uchimbaji wa madini
ulichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika maeneo mengi
Vijini vinavyozunguza Mto Zigi unaounganisha Wilaya za Muheza, Mkinga na
Tanga.
“Kufuatia
hali ya uharibifu wa vyanzo vya maji katika maeneo hayo, mwaka 2009
tuliamua kutumia fursa ya utafiti kupitia filamu kwa kuwasiliana na
wadau mbalimbali wa mazingira kwa ajili ya kutoa elimu na kuendesha
tafiti ili kuonyesha hatua zinazopaswa kuchuliwa katika kulinda na
kuhifadhi vya maji ya Mto Zigi” anasema Mhandisi Mgeyekwa.
Kwa
mujibu wa Mhandishi Mgeyekwa anasema tangu kuzinduliwa kwa filamu hiyo
mafanikio mbalimbali yameweza kupatikana ikiwemo uanzishaji wa Umoja wa
Wakulima Wahifadhi Mazingira Kihuhwi Zigi (UWAMAKIZI) ambapo jumla ya
vijiji 8 vimejiunga katika Umoja huo ulioanzishwa mwaka 2013 kwa ajili
ya ulinzi wa ardhi, maji na mazingira katika eneo la vyanzo vya Mto
Zigi.
Umoja
huu ulianzishwa mwaka 2013 ukihusisha vijiji 5 ambavyo ni Kimbo,
Shembekeza, Mashewa, Bombani na Kwaisaka ukiwa na wanachama 473 na hadi
Juni 2016 UWAMAKIZI ulikuwa na jumla ya wanachama 610 kutoka vijiji 8
vya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Mhandisi
Mgeyekwa anasema kutoka mwaka 2013-2016, TANGA UWASA kupitia
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imeupatia Umoja huo kiasi cha Tsh.
Milioni 100 kwa ajili ya kuendesha elimu ya kilimo hai na kilimo hifadhi
sambamba na kampeni ya uhamasishaji wa uhifadhi wa mazingira.
Anasema
hadi kufikia Juni 2017 kupitia juhudi za Umoja huo, jumla ya miti
3,196,174 imeoteshwa na kupandwa katika maeneo yote yanayozunguka vijiji
vilivyopo ndani ya mradi ikihusisha miti ya mbao, matunda, viungo na
miti rafiki na maji.
Akifafanua
zaidi Mhandisi Mgeyekwa anasema kupitia utafiti wa filamu mwaka 2016,
Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) zimeanza utekelezaji wa
mradi wa miaka (2016-2020) wa uhifadhi wa mazingira katika Bonde la Mto
Wami na Bonde la Mto Zigi.
Anaongeza
kuwa mradi huo umetengewa kiasi cha Tsh. Milioni 180, ambapo mpaka sasa
kiasi cha Tsh. Milioni 80 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi
huo ikiwemo kutandaza mabomba na kufunga viunganishi kwa ajili ya
kusambaza maji kwa wananchi waliopo katika vijiji vya Mashewa, Kimbo na
Shembekeza waliopo katika umbali wa kiomita 2.5 kati ya kilometa 6.5
zinazohitaji.
“Mradi
huu pia utasaidia kujenga malambo ya kunyweshea mifugo katika eneo la
Bwawa la Mabayani ili kuzuia mifugo kunywa maji moja kwa moja kutoka Mto
Zigi, ambapo kaisi cha Tsh. Milioni 50 tayari zimetengwa” anasema
Mgeyekwa.
Sote tunafahamu kuwa asilimia 75 ya uso wa dunia ni maji na asilimia 70 mpaka 75 ya mwili wa binadamu pia inachukuliwa na maji, kuhakikisha kuwa utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji unaendelezwa kwa ushirikiano na mipango ya pamoja.
No comments:
Post a Comment