• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 5 July 2017

    MANISPAA YA UBUNGO YAANZISHA REJESTA YA WAKAZI KWA KILA MTAA



    Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali muda mchache mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM. Leo June 5, 2017
     Mfano wa Fomu ya huduma kwa mwananchi (Fomu ya malalamiko)


    Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika Manispaa ya Ubungo.Leo June 5, 2017



     Kitabu cha Kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika ofisi za serikali

    Mkurugenzi
    wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa
    kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika
    Manispaa ya Ubungo.
    Leo June 5, 2017

     Mfano wa Fomu ya Rejista ya Wakazi katika kila Mtaa

    Ili kupunguza uhalifu katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam imebainika kuwa ni vyema kuwatambua wananchi wote na mahali wanapoishi
    ikiwemo kubaini wageni wote wanaowasili katika Manispaa ya Ubungo ikiwa ni pamoja na mahali wanapofikia.
    Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba Chama Jijini Dar es salaam.
    Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa  kumekuwa na uhalifu kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali Katika Manispaa hiyo jambo ambalo limetafutiwa muarobaini kwa kuanzishwa daftari la wakazi litakalobainisha wakazi wote ili kukitokea uhalifu iwe rahisi kuwabaini wahalifu hao.
    Kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya Wakazi wa Mtaa ni agizo lililotolewa hivi karibuni na MKUU
    wa Wilaya ya Temeke Mhe
    Felix Lyaviva
     
    kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa za
    Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni na Ubungo 
    wakati akihutubia kwa niaba
    ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda katika ufunguzi wa semina ya
    mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili kuwaelimisha watumiaji wa Intaneti wapatao
    milioni 20 sambamba na watumiaji wa simu za mikononi wapatao milioni 40 kuwa na
    matumizi bora ya simu za mikononi na mitandao ya kijamii.
    Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amesema kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya wakazi wa Mtaa pia kutakuwa na Fomu ya Rufaa ya Malalamiko katika kila Mtaa sambamba na kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali.


    Tayari vitabu hivyo vyote vimeanza kugawanywa katika kila Mtaa ili kuanza utekelezaji wa zoezi hilo haraka iwezekanavyo.
    IMETOLEWA NA:
    KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO 
    HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI