Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza katika Mkutano wa Wajasiriamali Wilaya ya Mkuranga juu ya kujiwezesha kiuchumi kutokana na ardhi walio nayo.
Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na wanawake wajasirimali wa Mkuranga juu fursa zilizopo katika Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkurnga, Abdallah Ulega akizungumza na wanawake wa Wilaya hiyo juu kutumia maada za mkutano katika kuzifanya fursa.
Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde (wa kwanza kulia )akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga, Mariam Abdallah, katika Mkutano wa Wajasiriamali mkoani Pwani.
Sehemu ya Jukwa la wanawake walikuwapo katika mkutano huo ulifanyika Mkuranga.
…………………………………………………………………………………
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amewatahadharisha wananchi wa wilaya hiyo kuacha kuuza ardhi hovyo na badala yake kuyatumia maeneo hayo katika kufanya shughuli za uchumi.
Mkuu wa Wilaya aliyasema wakati wa Mkutano wa Wanawake 402 Jukwaa Wanawake wa Wilaya ya Mkuranga ulioandaliwa na Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji Kiuchumi , amesema
kuwa wananchi wa Mkuranga wakiitumia ardhi vizuri itawapa maendeleo na sio kuuza na kwa ajili ya kucheza ngoma.
kuwa wananchi wa Mkuranga wakiitumia ardhi vizuri itawapa maendeleo na sio kuuza na kwa ajili ya kucheza ngoma.
Amesema Mkuranga ina ardhi ya kutosha yenye rutuba lakini wananchi wanashindwa kuitumia katika kujiletea maendeleo na kufanya kuwa na maisha magumu ya kujiendeesha kiuchumi.
Aidha amesema mkutano wa wanawake wajasiriamali uwe chachu katika kuanza kuitumia ardhi katika shughuli za kilimo na mazao watayoyalima watapata masoko.
Nae Balozi wa Heshima wa Sheli sheli, Maria Paul amesema kuwa wanawake walime matunda Passion na Nanasi na kuweza kuyanunua mwenyewe hivyo hawatakuwa na usumbufu wa soko kwa matunda hayo.
Maria amesema kuwa wananchi wa Mkuranga wamepata bahati ya ardhi lakini ardhi hiyo haitumiki katika kuwapa maendeleo wakiwemo wanawake wa wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wajasiriamali Wilaya ya Mkuranga, Mariam Abdallah amesema wakati wa maendeleo umefika wakutumia ardhi katika kuwaletea maendeleo.
Kwa Upande wa Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa kuna maendeleo yamewafikia wananchi iliyokuwa changamoto ikiwemo maji ambapo visima nane vimechimbwa katika vijiji vya Kimazichana Magharibi, Mkerezange, Midimuni,Ngole , Mwanambaya ,Yava
yava pamoja na Mlaleni.
yava pamoja na Mlaleni.
Aidha Mbunge ameomba kwa Mkuu wa Wilaya kutumika kwa Kituo cha Mti Pesa kwa abiri kushuka na kupanda ikiwa na biashara katika mida jioni ambapo Mkuu wa Wilaya alikubali na kusema jumatatu kituo hicho kitatumika.
Amesema kuwa vijiji vyote vitapata umeme katika mradi umeme vijiji awamu ya tatu na upande barabara ya lami kutoka Mkuranga Mjini kwenda Hospitali ya Wilaya Kupitia ofisi ya Mkuu wa
Wilaya hadi Halmashauri.
Wilaya hadi Halmashauri.
Ulega ameomba barabara Vikindu Viazi hadi Marogoro, Sangatini pmoaja na Barabara ya Kiguza , Hoyoyo , Kitonga kuingia katika barabara za Mkoa ili kutokana na fursa za maendeleo ya maeneo hayo
No comments:
Post a Comment