Mkuu Wa Mkoa Wa Dar es salaam Leo amekutana na ujumbe Wa walimu 18 kutoka nchini marekani ambao Wapo hapa nchi kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo utamaduni, lugha ya kiswahili na namna ya kuandaa mitaala.
Walimu hao ni Pamoja na Wa washule za Msingi na Sekondari Wapo katika hatua ya mwisho kumaliza mafunzo yao hayo.
Miongoni mwa masuala waliyozungia wakati Wa mkutano wao huo ni Pamoja na kuangalia namna ya kujenga maktaba ya jamii mkoani Dsm ambayo itawezesha wananchi kupata fursa ya kujisomea na kuelewa utamaduni Wa nchi hiyo na ndani ya nchi.
Kufuatia mikakati hiyo ya ujenzi Wa maktaba Makonda amewahimiza wananchi Wa Mkoa huo kujenga utamaduni Wa kujisomea.
Jambo lingine ambalo wamelijadili ni Pamoja kuangalia wanajenga vipi umoja ktk kuleta walimu watakao kuja kufundisha mkoani humo ili vijana wapate uelewa wa kutosha
No comments:
Post a Comment