BAADA ya kuvumilia kwa muda mrefu wananchi wa Jimbo la Tumbe wakifikiria kwamba huenda
mwakilishi wao waliyemtuma kuwawakilisha kwenye Baraza la Wawakilishi
ataweza kushirikiana nao katika kuwatatulia kero na changamoto
zinazowakabili hatimaye wamevunja ukimya na kutupa lawama nzito kwa
mwakilishi huyo
Wamesema
kwa kipindi chote hicho wananchi hao wamekuwa wavumilivu hatimaye
wameshindwa kujizuia na kutoa malalamiko lakini bado jitihada hizo
hazijazaa matunda.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi wamesema kiongozi muajibikaji ni yule ambae
huwa tayari kushirikiana na wananchi wake ili kuweza kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabli sambamba na kutathmini mendeleo yaliyopo .
Wameeleza
kwamba kitendo cha kuwakimbia wananchi baada ya lengo la kupatiwa kura
kukamilika sio suluhuhisho bora kwa kiongozi mwenye kujali maslahi kwa
wananchi waliomchagua.
Hali
hiyo ni tofauti kwa mwakilishi wa jimbo la Tumbe Ali khamis Doholo
ambae amelalamikiwa na wananchi wa jimbo hilo kwa kukwepa kutekeleza
majukumu yake ambayo aliyaahidi kabla ya kuchaguliwa
“Awali
tulikuwa na matumaini kwaba tumepata kiongozi ambae ataweza kuzitatua
kero zetu kutokana na ahadi alizozitoa wakati wa kampeni lakini baada ya
kuchaguliwa tu kiongozi huyo amegeuka kakakuona ndani ya jimbo
haonekani wala hasaidii shuhuli za maendeleo ”alisema.
Aidha
waandishi wa habari walipofanya jitihada ya kumtafuta kwa njia ya simu
kutaka maelezo hakua tayari kutoa ushirikiano akidai akiwa tayari
atawatafuta.
Mwakilishi
wa wananchi wa Jimbo la Tumbe amekuwa na kawaida ya kuwakwepa wandishi
wa habari wanapohitaji kupata maelezo juu ya malalamiko ya wananchi
waliomchagua jambo ambalo linakwamisha kupatikana taarifa za maendeleo
katika Jimbo hilo .
“Mimi
binafsi nimekuwa nikisumbuka sana kumtafuta Mwakilishi wa huyo , lakini
juhudi zangu zimeshindwa kuzaa matunda baada ya kuendelea kupigwa
danadana ”alisema mmoja wa wandishi wa Habari .
Wananchi
hao wamemuomba naibu Katibu Mkuu wa CCM Abdlaa Juma Mabodi kufanya
ziara ya kikazi katika Jimbo ili kusaidia kuhoji utekelezaji wa ahadi za
mwakilishi alizozitoa wakati akiomba kura .
Wamesema
kitendo cha Naibu Katibu Mkuu wa CCM kufanya ziara katika jimbo hilo
kunamfanya Mwakilishi wao aone aibu kutokana na kitendo chake cha
kuwakimbia wapiga kura wake
No comments:
Post a Comment