• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 1 July 2017

    UTAFITI UNAONYESHA KUWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 WILAYA YA MONDULI IMEATHIRIWA NA MMOMONYOKO WA ARDHI,WANANCHI WASHAURIWA KULIMA KILIMO HIFADHI

    Watafiti
    kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Uingereza vya Plymounth,Exeter,na
    Schumacker wakiwa wanamsikiliza kwa makini mkalimani ambaye ni  ndugu
    Sitayo aliyevaa (miwani ) katika warsha ya Wadau wa Jali Ardhi
    iliyofanyika Chuo Cha Ualimu Monduli.Picha na Vero Ignatus
    Blog
    .

     
    Wakwanza
    kushoto ni Profesa Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na
    Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akiwa anafuatilia kwa karibu Profesa
    William Blake kutoka nchini Uingereza akipanda mti katika eneo la chuo
    cha Ualimu Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog



    Mtafiti
    kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akitoa
    elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku
    mbili wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
    Mtafiti
    kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela
    Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi
    akitoa elimu
    kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili
    wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.

     
    Profesa Willium Blake akifuatilia
    kwa makini kinachoendelea katika Warsha hiyo.Picha na Vero Iganatus
    Blog.
     
    Zoezi la upandji Miti likiwa
    likiendelea kwa wageni kutoka vyuo vikuu vitatu nchini
    Uingereza vya Plymounth,Exeter,na
    Schumacker wakishirikiana na Dkt Kelvin Kimei (anayeandika
    )kutoka 
    Taasisi ya Sayansi na
    Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha

    .Picha na Vero Ignatus Blog.

     Mtafiti
    kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela
    Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi
    akitoa elimu
    kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili
    wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus
    Blog.
     Profesa
    Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson
    Mandela Arusha akiwa anatoa ufafanuzi wa jambo katika warsha ya
    Mradi wa Jali
    Ardhi kwa wadau waliohudhuria katika Chuo Cha Ualimu
    Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
     Profesa William
    Blake kutoka nchini Uingereza
    akitoa neno la shukrani baada ya kumalizika kwa warsha ya siku mbili
    iliyowakutanisha wadau wa
    Mradi
    wa Jali Ardhi aliyesimama kushoto kwake ni Charles Bonaventure kutoka
    Taasisi isiyo ya kiserikali ya ECHO.Picha na Vero Ignatus
    Blog.

     Na.Vero Ignatus
    .Monduli
     
    Wananchi
    wa monduli wameaswa kulima kilimo cha uhifadhi ili kuhifadhi  mazingira na kuepusha kutokea
    kwa mmomonyoka

    wa ardhi katika maeneo yao  na kudhibiti makorongo yakiwa
    katika hatua za
    awali.
     


    Hayo
    yamesemwa na
    Issakwisa Ngondya mtafiti
    kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  Arusha ambapo amesema kuwa
    zaidi ya asilimia
    50
    katika wilaya ya Monduli imeathiriwa na mmomonyoko wa ardhi
    .
     


     Ameainisha vijiji
    vilivyoathirika zaidi ni
    pamoja na Emaerete,Lendikinya,Arkaria,Orchoropus ,Likamba,Oletushora pamoja na
    Nangungwa,amesema kutokana na uharibifu  huo wa ardhi
    umesababisha rutuba kupotea katika ardhi na husababisha upatikanaji hafifu wa
    mazao kwa mkulima.

     
    Amewataka wadau hao
    k
    uhifadhi uoto  kwa
    kuotesha mimea na miti

    ili kuzuia udongo usisombwe na maji au upepo kwani  ardhi iliyofunikwa
    ni madhubuti zaidi dhidi ya mmomonyoko wa udongo kuliko ardhi ambayo
    haijapandwa kitu amesisitiza  kupanda mazao ya kudumu na kupanda mazao
    yanayofunika ardhi.
     




    Nae Profesa
    William Blake
    kutoka nchini Uingereza
    amesema kuwa amefurahishwa sana na matumaini makubwa waliyonayo wana
    Monduli kwaajili ya
    kurudisha ardhi liyokuwa imeharibika  kwa mafanikio makubwa kwani warsha
    hiyo ina umuhimu mkubwa kwa watu wote wa sasa na kwa vizazi vijavyo
    pia
     
    Kwa upande wake Profesa
    Patrick Ndakidemi
    amesema akiona mashamba
    yameharibika huwa anajisikia vibaya kwani bila ardhi hakuna maisha amewataka
    washiriki wote kuyatendea kazi yale yote waliyojifunza ambapo
    amewataka wadau hao kuwa mfano bora  katika maeneo
    yao.



    Akitoa neno la shukrani kwa
    niaba ya serikali 
    Afisa
    kilimo na ushirika na umwagiliaji Ridhiwani kombo kutoka
    halmashauri ya Monduli
    amewashukuru waliofanya utafiti na kurudisha majibu kwani wengine huwa
    wanafanya utafiti lakini hawarudishi majibu,amesema utafiti walioufanya
    utatumika katika maeneo m
    engine hapa nchini.
     
     Kwa upande wawashiriki akitoa
    neno la shukrani katika semina hiyo ya siku mbili Adiso Matayo kwa niaba
    yawengine amewashukuru wawezeshaji kwa
    kuwapatia elimu ambayo ni faida kwao na kwa kizazi kijacho amesema elimu
    waliyoipokea wataifanyia kazi

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI