Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa
Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka Kaimu Mkurugenzi wa
Masoko na Utafiti , Angela Mziray katika banda la NHIF katika maonesho
ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es
Salaam.
…………………………………………………………………………..
Na. Frank Mvungi
Vituo vya afya vinavyo milikiwa
na Serikali vimetakiwa kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ili
kusogeza huduma za afya karibu na wananhi.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF ambaye pia ni Spika Mstaafu, Anna
Makinda, baada ya kutembelea Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere.
Makinda alieleza kuwa dhamira ya
Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anafikiwa na huduma ya Bima
ya Afya kupitia mfuko huo.
“Mfuko wa Bima ya Afya haufanyi
biashara na niseme tu kwamba tunachokifanya ni kutoa huduma kwa kuunga
mkono juhudi za Serikali kuhakikisha kuwa huduma za afya hapa nchini
zinaimarika na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi”, alieleza Makinda.
Alieleza kuwa Mfuko huo umekuwa
ukitoa mikopo ya vifaa tiba, dawa pamoja na nyenzo nyingine kusaidia
kuboresha huduma za afya hasa katika hospitali na vituo vya kutolea
huduma za afya vilicyosajiliwa na mfuko huo.
Pia mama Makinda amewaasa
Watanzania kujiunga NHIF ili wanufaike na huduma na pia kuepuka usumbufu
pale wanapougua kwani kwa kufanya hivyo watakuwa pia wanaunga mkono
juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kila Mtanzania
anapata huduma bora za afya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga alieleza kuwa mpaka sasa kuna jumla ya
vituo vya afya 6,998 nchi nzima ambayo vinatoa huduma za afya kupitia
NHIF na kwamba katika kipindi hiki cha maonesho ya Saba Saba pekee Mfuko
huo umesajili watoto 1,450 kupata huduma za afya.
Mfuko wa Bima ya Afya umekuwa
ukiwahahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko huo ili kuwa na uhakika wa
kupata matibabu pale wanapougua.
No comments:
Post a Comment