Mkuu wa Operesheni Maalun za
Jeshi la Polisi, Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas akiwa
katika eneo la tukio akizungumzia namna Jeshi la Polisi lilivyofanikiwa
kuuawa watu wawili awanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu
wanaojihusisha na mauaji watu katika Ikwiriri na kibiti. (Kushoto
kwake ) ni Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi Rufiji, Kamishina
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga akiwa ameshika
silaha aina ya Rifle 375 iliyokutwa katika eneo la tukio. Picha na
Tamimu Adam.
…………………………………………………………………………
Na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini
limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa
wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya kipolisi Rufiji
ambapo mmoja kati ya watu hao ametambulika kwa jina la Abdallah Ally
Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda
mrefu kutokana na kushiriki kwake katika matukio ya mauaji maeneo ya
Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri.
Akielezea tukio hilo, Mkuu wa
Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi
Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19,
julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la Utende kata ya Ikwiriri,
wilaya Rufiji kanda maalum ya Polisi Rufiji.
“ Askari Polisi wa doria
waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walianza
kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia askari kwa
risasi, askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa
kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki
wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu
iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.
Aliongeza kuwa katika eneo hilo
la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo ilikutwa
imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2). Aidha, Miili ya
marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali
ya Taifa ya muhimbili.
Kamanda sabas ameendelea kutoa
wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa
taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba
opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi
Rufiji ni endelevu na hakuna atakaye baki
No comments:
Post a Comment