Balozi wa Japani nchi Tanzania,
Masaharu Yoshida akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi
wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Bibi Amina Masenza.
Balozi wa Japani nchi Tanzania,
Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la
Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya
sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa
Richard Kasesela.
Balozi wa Japani nchi Tanzania,
Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la
Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya
sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa
Richard Kasesela.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa mbele.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa nyuma.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa ndani.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa
shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule
ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa
shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule
ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Eneo la kunawia lililo ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
………………………….
Na Hassan Mabuye
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ismani
Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan amesaidia ujenzi wa
bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa
Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi Iringa Balozi wa
Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo
inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono
shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania.
Ubalozi huo wa Japan ambao
umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi
umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Isimani Mhe. Wiliam
Lukuvi aliyoyaomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali la
shule hiyo kuteketea kwa Moto.
Balozi huyo alisema kuwa mkataba
wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February
mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za
kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.
Ubalozi wa Japan nchini Tanzania
umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya
mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada
za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.
“waziri Lukuvi lileta maombi ya
miradi mbalimbali ambayo miongoni mwake ni kujengewa Hostel ya wasichana
ya shule ya Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka 2008,
kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na
mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa, kwa hiyo
namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo”
“Leo nimefurahi kuona ujenzi
umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya kutosha, mfumo wa kuhifadhi
maji wa Hosteli hii umekamilika ikiwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 208
kama kusudio la ujenzi, na ni matumaini yangu mradi huu utatunzwa vema”
Balozi huyo alisema kutokana na
usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo Corporation kampuni ya
kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu ya mionzi ya jua kwa
ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika bweni hilo.
Hata hivyo alisema ubalozi wa
Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania
chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema kuwa serikali ya mkoa
inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia kupunguza msongamano ya
wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo litatunzwa vizuri.
Waziri Lukuvi pamoja na kupongeza
msaada huo wa kujengewa bweni na miradi mingine amewataka wanafunzi hao
kutunza mabweni hayo na kujiepusha na hatari zozote za kuchoma moto,
kitendo ambacho kinasababisha upotevu mkubwa wa mali na uhai wa
wanafunzi hao
No comments:
Post a Comment