Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dk. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika mkutano wa kuzindua mpango wa
kuzitembelea hospitali za umma nchini ili kujua mafanikio na changamoto
zilizopo kwenye hospitali hizo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima wa wizara hiyo. Mpango huo
umeandaliwa na wizara ya afya na ziara hiyo imeanza rasmi leo Muhimbili.
Baadhi
ya wataalamu wa afya kutoka Muhimbili na taasisi nyingine wakimsikiliza
Katibu Mkuu, Dk Ulisubisya katika mkutano wa uzinduzi uliofanyika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru
akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa mpango wa kutembelea hospitali za
umma ili kujua mafanikio na changamoto zilizopo kwenye hospitali hizo.
Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga wa Muhimbili
akimwelekeza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima
(kushoto) wa wizara ya Afya wakati wa ziara ya kutembelea hospitali hiyo
leo. Wengine ni maofisa kutoka wizara ya afya na hospitali ya
Muhimbili.
………………………………………………………………………….
Wizara
ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezitaka
hospitali nchini kutumia miongozo katika kutekeleza shughuli mbalimbali
za huduma za afya pamoja na kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuwapo kwa
mawasiliano kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na hospitali
nyingine za rufaa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulisubisya wakati
akizindua mpango wa kufuatilia utoaji wa huduma za afya yakiwamo
mafanikio na changamoto katika hospitali za umma nchini.
Dk
Ulisubisya amesema mpango wa wizara yake ni kuzitembelea hospitali za
umma nchini utaanzia kwenye hospitali za kibingwa ili ziwe kitovu cha
kutoa mafunzo kwa hospitali nyingine nchini.
“
Malalamiko ni mengi yanapaswa kushughulikiwa kwa kuwekwa mifumo imara
ya utekelezaji wa shughuli za huduma za afya kwa lengo la kuzuia kushuka
kwa ubora wa huduma. Pia, hali hii itasaidia kuimarisha maadili
miongoni mwa watumishi,” amesema Dk Ulisubisya wakati akizindua mpango
huo leo.
Amesema
wizara ya afya itaendelea kushirikiana na kitengo cha elimu ya afya kwa
umma ili kuhakikisha watumiaji wa huduma za tiba wanafahamu mfumo na
taratibu za upatikanaji wa huduma za tiba katika ngazi mbalimbali ili
kuondoa usumbufu na malalamiko kutoka kwa wagonjwa.
Akizungumzia
maslahi ya wafanyakazi, amesema serikali inafanyia kazi maombi ya
kuboreshwa kwa maslahi yao na kwamba wachape kazi kwani inakumbuka suala
hilo.
Pia,
Dk Ulisubisya aliipongeza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa juhudi
kubwa ya kuboresha huduma za afya kwa kupanua huduma za afya, kusomesha
wataalamu wa afya na kununua vifaa tiba.
“Muhimbili mnafanya kazi nzuri na kubwa, naamini taasisi nyingine zitajifunza kwenu, mna mambo makubwa ya kujivunia,” amesema.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima amefafanua lengo la ziara
yake ni kuwezesha kupatikana kwa taarifa kwa wakati na utasaidia katika
utekelezaji wa huduma za afya katika hospitali nchini.
Dk. Gwajima amesema kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa wa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Kutakuwa
na ratiba ya kudumu ya vikao kati ya wizara na watoa huduma kuhusu
utekelezaji wa huduma za tiba. Taarifa za halmashauri lazima zikutane
ili kujua hali za huduma za afya kwenye halmashauri zenu, hivyo kutakuwa
na kamati mbalimbali ili kuwasilisha ufuatiliaji wa shughuli za huduma
za afya.
Mkurugenzi
wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akizungumzia juhudi za kuboresha
huduma za afya, amesema kuwa upatikanaji wa dawa MNH ni asilimia 95
kutoka asilimia 40. Pia, amesema Muhimbili inatarajia kupata wataalamu
18 kutoka Cuba wa masuala ya mionzi, usingizi, macho na masikio.
Pia,
Profesa Museru ameiomba serikali kuipatia Muhimbili kibali cha kuajiri
wataalamu mbalimbali kwa kuwa ina upungufu wa wafanyakazi karibu 300
kutokana na baadhi ya wafanyakazi kustaafu, kupoteza maisha na wengine
130 kubainika kuwa na vyeti feki.
Ziara
hiyo imeanza rasmi leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na maofisa
wa wizara hiyo wametembelea Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali, Idara
ya Maabara Kuu na idara mbalimba ambako wamezungumza na wafanyakazi
pamoja na wagonjwa
No comments:
Post a Comment