• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 18 August 2017

    BI REHEMA; Angusha kilio kwa Rais Magufuli


    Bi. Rehema Juma Kishena kama anavyoonekana pichani na uvimbe 
    unaomsumbua kwa miaka 17 sasa.


    Mwanamke mmoja mkazi wa  Levolosi Arusha  bi Rehema Juma Kishena (40) amemuomba Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania pamoja na  watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia kupata fedha ya matibabu kutokana na tatizo la uvimbe linalomsumbua katika shavu lake la kulia ambalo limezunguka taktibani robo tatu ya uso wake .

    Mwanamke huyo ambae ni mama wa watoto (4) amesema kuwa tatizo hilo lilimuanza kwa jino kuumua ,akachukua hatua ya kwenda hospitalini kuling’oa , mwaka 2001  uvimbe ulijitokeza katika jino alilong’olewa, na kupelekea kufanyiwa  upasuaji, baada ya miaka mitatu uvimbe
    ulirudi tena kama awali.

    ‘’Jino lilikuwa linaniuma nikaenda hospitalini kuling’oa, ndipo ukaanza uvimbe kwenye jino nililongoa nikarudi hospitalini wakaniambia nifanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe ,baada ya miaka mitatu tatizo hilo likajirudia kama lilivyokuwa mwanzo “alisema Bi. Rehema.

    Amesema kuwa kwa sasa hana msaada wowote kwani wazazi wake ni wazee, hawana mwezo wa kumsaidia,yeye mwenyewe hana mume kwani alimkimbia wati alipoona tatizo linaendelea kuwa kubwa.

    “Nawaombeni msaada ili niweze kujitibu kwani hali yangu kama mnavyoiona nipo kwa dada yangu hapa ,sina msaada wowote” alisema Bi. Rehema.

    Kwa upande wake dada yake ( Rehema )Aziza Bakari Muyai amewaomba watanzania kushirikiana nae katika kumsaidia mdogo wake ili aweze kupatiwa matibabu kwani hali yake inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda.

    Ameomba kwa yeyote aliyepo tayari kumsaidia atumie mawasiliano kwa namba 0653179373.
    Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake wa ( 3) Sophia Dastan Mandia nyumbani kwa dada yake Levolosi mkoani Arusha. Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake Sophia Dastan Mandia pamoja na dada yake bi Aziza Bakari Muyai nyumbani kwake Levolosi Mkoani Arusha

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI