• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 17 August 2017

    DHAMANA YA MTUHUMIWA WA AFRIKA KUSIN, TSAMPOS KUJULIKANA KESHO.


    MAPEMA hii leo, upande wa Mashtaka katika kesi
    inayomkabili raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61), umeileza mahakama
    kuwa, mshtakiwa huyo hana uhalali wa kuishi nchini ingawa imethibitika kuwa ni
    kweli ana makazi eneo la mbezi jiji Dar es Salaam.


    Wakili wa Serikali Nassoro Katuga amesema hayo mbele
    ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
    alipokuwa akiwasilisha ripoti ya ya mahakama iliyowaagiza kwenda kukagua makazi
    ya mshtakiwa pamoja na hati ya mshtakiwa.
    Image result for bendera afrika kusini

    Amesema, kamishna wa Uhamiaji nchini amethibitisha
    kuwa Tsampos, hana uhalali wa kuishi nchini ila Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
    wa Mbezi amethibitisha kuwa, mshtakiwa huyo ni kweli anayo makazi ya kuishi
    eneo hilo.

    Hata hivyo, wakili wa utetezi, Jebra Kambole,
    ameomba mahakama kumpatia dhamana mshtakiwa huyo kwani imedhihirisha kuwa ni
    kweli mshtakiwa anaishi Mbezi na pia Kamishna wa Uhamiaji hajaeleza ni kwa nini
    hana uhalali wa kuishi hapa nchini.

    Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kwa ajili ya
    kutolewa uamuzi kama apatiwe dhamana au la.

    Raia huyo wa Afrika Kusini, anakabiliwa na mashtaka
    ya kutishia kwa mtandao, kuishi nchini kwa muda wa miaka minne bila kibali na
    kutumia paspoti yenye visa ya kugushi.
     Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) aliyekuwa anashikiliwa kwa makosa manne leo tena amesomewa mashtaka katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, mashtaka yake ikiwemo kuishi nchini bila kibali.  Leo pia  imethibitishwa kuwa Visa yake ya kusafiria si halali na hana uhalali wa kuishi hapa nchini.
     Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61)akiwa amejificha sura yake katika mahakama ya Kisutu jijini  Dar es Salaam

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI