Wizara ya afya nchini Sierra Leone imebainisha takriban nusu ya maiti 400 zitokanazo na maporomoko ya udongo na mafuriko nje ya mji wa Freetown tayari zimezikwa na watu mia sita bado hawajulikani walipo.
Serikali ilisema mazishi ya pamoja yangeahirishwa hadi leo ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kutambua miili ya maiti hao na kuwaaga pia rais wa nchi hiyo ametangaza siku saba za maombolezi.
Lakini mkuu wa wataalamu wa magonjwa kutoka mjini Freetown ameiambia BBC kwamba baadhi ya mazishi teari yameshafanyika yenye kujumuisha maiti ambayo tayari zimetambuliwa au zilizokuwa zimeharibika kabisa.
Nathaniel Williams ni daktari katika hospitali kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya miripuko kama vile kipindupindu.
Ameongeza kusema kuwa hivi sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea
No comments:
Post a Comment