• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 30 August 2017

    Meya Wa ubungu atema Chechen

    MEYA UBUNGO AMALIZANA KWA AMANI NA WAMACHINGA KUPISHA UJENZI WA FLYOVER UBUNGO

    Leo tarehe 30 August 2017, Mstahiki Meya wa Halmashauri Ya Manispaa Ya Ubungo,amefanya mkutano wa hadhara akihutubia wamachinga,katika makutano ya Ubungo Mataa.Akiambatana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bw.John Kayombo pamoja na Maofisa kutoka ofisi za TANROANDS,JESHI LA POLISI,WIZARA YA UJENZI, MKANDARASI WA FLYOVER UBUNGO- CCI-CCE,
    Wenyeviti serikali za mitaa na watendaji wa kata za Makuburi,sinza na Ubungo.
    Ikiwa dhamira yake ni Kuzuia Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwaondosha kwa Nguvu wa Machinga katika makutano ya Ubungo mataa,baada ya Kulalamikiwa na Mkandarasi wa FLYOVER UBUNGO,kuwa wamezagaa sana katika maeneo hayo kiasi cha kukwamisha Ujenzi wa Mradi ikiwemo kukosa eneo la kuweka vifaa vyao kama ,vifusi na Mitambo ya Ujenzi katika Eneo hilo.
    Akiongea katika mkutano huo ,Mstahiki Meya amewaomba Wamachinga wapishe kwa Amani ishara kumuunga Mkono yeye (Meya) katika jitihada za Wamachinga kushughulikiwa kero zao bila ya Jeshi la Polisi kuwapiga Mabomu,
    Aidha amewaruhusu wamachinga kwenda kupanga biashara zao popote pale barabarani nje ya eneo la Mradi, watakapo ona inafaa bila ya kubughuziwa na mtu yeyote,kufuatisha kauli ya Mheshimiwa Rais Kuwa Wamachinga wasisumbuliwe ,na Kwa Wale watakao taka kurejea kituo cha Mawasiliano,Manispaa ya Ubungo imeandaa utaratibu Mzuri wa Kuponi Maalumu kwa Wamachinga wa Ubungo.
    Pamoja na kujadiliana changamoto mbalimbali na Wamachinga Viongozi wamekubali kuwaongezea siku tatu Mbele Wamachinga ilikujipanga namna ya kuondoka Eneo la Mradi,Na pia baadhi ya wamachinga wameomba kazi za vibarua katika Mradi kwa kipindi ujenzi utakapoendelea,huku Mama lishe wameruhusiwa kubaki kuwapikia Mafundi katika Mradi kwa utaribu Maalum kama Fursa ya Kipekee kwa kina mama hao

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI