• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 24 August 2017

    NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI, DKT. ALOYCE NZUKI AFUNGUA WARSHA YA KUKUSANYA MAONI YA WADAU WA KANDA YA KATI KWA AJILI YA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA UTALII YA MWAKA 1999 MJINI DODOMA

    Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na
    Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja
    ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya
    Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
    ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma
    leo. 
     
    Dkt. Nzuki amesema
    ipo haja sasa kwa Sekta za Umma kuona umuhimu wa kuwekeza moja kwa moja katika
    biashara ya utalii nchini hususani katika huduma za malazi na usafiri ili
    kuiwezesha Serikali kupata mapato ya moja kwa moja na kuongeza zaidi kwenye pato la
    taifa. 
     
    Alisema kwa kuimarisha usafiri wa anga kutawezesha usafiri wa watalii
    moja kwa moja kutoka kwenye soko na kuwaleta nchini huku wakilipia gharama zote
    hapa nchini tofauti na hivi sasa ambapo baadhi ya makampuni ya nje hulipwa
    fedha kiasi nje ya nchi na hivyo kuikosesha Serikali mapato kupitia ushuru
    unaotozwa na TRA. 
     
    Alisema sio lazima Serikali iwe inasimamia moja kwa moja
    utoaji wa huduma hizo kwa kuwa upo uwezekano wa kutumia makampuni makubwa hata
    ya nje ya nchi kuja kuendesha huduma hizo kwa ufanisi zaidi hapa nchini.  
    Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na
    Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na wadau wengine wa sekta ya utalii wakimsikiliza
    Prof. Raphael Mwalyosi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia) wakati
    akiwasilisha mada kuhusu Hoja ya Marekebisho ya Sera ya Utalii ya Mwaka 1999
    katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kupitia upya Sera hiyo iliyoandaliwa
    na Wizara hiyo kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii mjini
    Dodoma leo.
    Kamu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya
    Maliasili na Utalii, Deograsias Mdamu akizungumza katika warsha ya siku moja ya
    kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya
    Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
    ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma
    leo. 
    Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
    Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (katikati waliokaa) na wadau wa sekta ya
    utalii katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya
    utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa
    na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho
    la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo.
    Baadhi ya wadau wa sekta ya utalii wakisikiliza moja
    ya mada katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya
    kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya
    Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii
    Tanzania mjini Dodoma leo. 
     Baadhi ya wawezeshaji wa hafla hiyo ambao ni Maafisa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha hiyo. 
    Baadhi ya wadau wa warsha hiyo wakisikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki. 
     Baadhi ya wadau wa warsha hiyo.
    Baadhi ya Washiriki wa warsha hiyo kutoka Mikoa ya Kanda ya Kati iliyofanyika mjini Dodoma. (NA HAMZA TEMBA – WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
    HOTUBA YA UFUNGUZI YA NAIBU KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, DKT. ALOYCE NZUKI
    HOTUBA YA KAIMU MKURUGENZI IDARA YA UTALII, DEOGRASIAS MDAMU

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI