Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge akifungua mafunzo kwa watumiaji wa Mfumo mpya wa Kielektroniki ulioboreshwa (PlanRep) yanayofanyika mjini Dodoma yakiwashirikisha Waganga Wakuu wa Mikoa,Halmashauri,Maafisa Mipango,Makatibu wa Afya,Wachumi na Wahasibu.
Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Erick Kitali akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kiongozi wa Timu ya Mifumo kutoka Kutoka mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bw. Desderi Wengaa akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Mfumo huo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mjini Dodoma.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo mara baada ya hafla ya ufunguzi.
Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo Dodoma.
……………………………..
Beatrice Lyimo- Maelezo,Dodoma
Watendaji wa wa Serikali wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma na weledi ili kuendana na dhana ya Serikali ya awamu ya Tano inayosisitiza uwazi na uwajibikaji katika kuwahudumia wananchi katika maeneo yakutolea huduma.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watumiaji wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na Ripoti (PlanRep)za Mamlaka za Serikali za Mitaa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.
“Sasa ni lazima watumishi wa umma katika maeneo yakutolea huduma mbadilike na muendane na Dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu inayosisistiza kutoa huduma bora zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi wa chini” Alisisitiza Bi Rehema
Akifafanua Bi Rehema amesema kuwa matokeo ya matumizi ya mfumo huo ulioboreshwa yanaonekana na yatagusa maisha ya wananchi wote katika maeneo yao kwa kuwa yatasaidia kuongeza tija na uwajibikaji hali itakayosaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
Aliongeza kuwa mfumo wa PlanRep ulioboreshwa utatumika kuanzia ngazi ya msingi yaani vituo vya kutolea huduma za kijamii ikiwemo Zahanati,Hospitali na Shule.
Mfumo huu wa kuandaa Mipango,Bajeti na Kutoa Ripoti utapunguza gharama kwa kiasi kikubwa zilizokuwa zikitumika awali kabla ya kuanza kwa mfumo huu mpya.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Mifumo ya TEHAMA kutoka mRadi wa PS3 Desderi Wengaa amesema kuwa lengo la mradi huu ni Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unatakekelezwa na Serikali ya Tanzania ukilenga kuimarisha Mifumo katika Sekta ya Umma ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali za Mitaa kwa Jamii hasa zile zenye uhitaji zaidi.
“Mradi huu unafanya kazi katika maeneo makuu matano ambayo ni Utawala Bora, Ushirikishwaji wananchi, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha, Mifumo ya TEHAMA pamoja na Tathimini na ufutiliaji” alisema Desderi Wengaa.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa, mfumo huu umesukwa na wataalamu wazalendowa hapa nchini na upo tayari kupokea mabadiliko kulingana na mahitaji ya wakati, na vilevile utasaidia kupunguza muda na gharama za uaandaaji wa Mipango na Bajeti.
Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma(PS3) ni mradi wa miaka mitano ulia mnamo Julai 2015 na kutarajiwa kukamilika Julai 2020 ambapo utarahisisha utendaji kazi na kusaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali.
No comments:
Post a Comment