Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo
amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo
kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa
Wakazi wa Dar es Salaam.
Katika
ziara hiyo Makonda ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa
Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya
kusafirisha na kutibu Maji taka.
Makonda
amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ni
kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia
Wananchi wote.
Amesema kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo
Vinne vikubwa vya usambazaji
wa Maji vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na
Bunju vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.
Katika
ziara hiyo pia Makonda ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye
Ziara ya Dar Mpya ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa
kuzalisha Lita 160000 ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.
Aidha Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo
kutajengwa
Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la
Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu
kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na Serikali
ya Japan.
Hata hivyo
amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha Wakazi
wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi
mbalimbali inayoendelea.
Amewataka
Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za
DAWASCO ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo
watawekewa utaratibu wa malipo.
 |
No comments:
Post a Comment