Mkurugenzi wa shule za almuntazir islamic school,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam.
huyu
ni katibu wa mshindano hayo yajulikanayo kama Mwalimu Nyerere school
invetation debate championship Bwn. Dominic Mwakifulefule.
hawa ni wanafunzi waliopata nafasi kushiriki katika mdahalo huo,wakati wakijadiliana ukumbini hapo.
hawa
ni baadhi ya wanafunzi walioshiriki mashindano hayo Mduduzi Mhlanga
kutoka Zimbabwe(kulia) pamoja na mwanafunzi kutoka alimuntazir(
kushoto).
Wanafunzi
250 kutoka katika shule mbalimbali za afrika kushiriki katika
Mashindano ya mdahalo yaliyoanza leo katika shule ya Almuntazur seminary
school, iliyopo jijini dar es salaam kwa lengo La kuwajengea wanafunzi
hao uzoefu wa kijieleza kwa kumjenga mwanafunzi katika kujiamini na
kuweza kufanya vizuri katika soko LA ajira.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkurungenzi wa shule zote za Almuntazir Islamic
school bwn. Mahmood Ladak, amesema , mashindano hayo ambayo
yameshirikisha shule 15 kutoka Tanzania na nyingine kutoka katika nchi
nyingine kama Zimbambwe,South Afrika pamoja na Uganda.
Amesema
kuwa kwa lengo LA mashindano hayo ni kuwakutanisha wanafunzi hao na
kutoka shule nyingine ili kunadilishana mawazo mbalimbali ya kielimu
waliojifunza darasani.
Mashindano
hayo yajulikanayo kama Mwl Nyerere school inventation debate
championship, yanayotarajiwa kumalizika August 13 mwaka huu.
katika
mjadala huo kuna mada mbalimbali ambazo wanajadili ikiwemo National
system na mada mbalimbali zinazohusu masomo na kuwapa fursa wanafunzi
hao kubadilishana mambo mbalimbali waliyojifua katika masomo yao.
Kwa upande wake Mratibu wa Mdahalo Dominic Mwakifulefule amesema katika kuandaa
mdahalo huu walitumia utaratibu wa kujiandikisha (process registration)
, mitando ya kijamii vyombo vya habari kwa lengo la kuhamasiaha
ushiriki wa shule.
Hata
hivyo wanafunzi walipata fursa ya kuzungumza kuhusiana na mashindano
hayo ambapo mwanafunzi Mduduzi Mhlanga kutoka katika shule ya st john
collage Zimbabwe amesema mashindano hayo ni mazuri kwani yanawajenga
katika kujieleza na kujiamini, naye mwanafunzi Hawa kutoka katika shule
ya Almuntazir iliyopo Tanzania ameshukuru uongozi wa shule hiyo kuandaa
mashindano kama hayo kwani yatawajenga kielimu katika masomo yao
No comments:
Post a Comment