Mwenyekiti aliyemaliza muda wake
EARATC Bw. Michael Muhoja kutoka TRA akikabidhi ngao na nyundo kama
ishara ya kumkabidhi vitendea kazi mwenyekiti mpya Bi. Martine Nibesumba
kutoka OBR Burundi.
Mwenyekiti mpya Bi. Martine akifungua kikao kazi cha EARATC mara baada ya kukabidhiwa rasmi uenyekiti.
Mwenyekiti mpya wa EARATC Bi. Martine Nibesumba kutoka OBR-Burundi
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja
…………………………..
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imekabidhi uenyekiti wa kamati ya ufundi ya masuala mbalimbali ya
utekelezaji katika Mamlaka za Mapato zilizopo ndani ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (East Africa Revenue Authorities Technical Committee). Katika
mkutano wa 80 unaoendelea tangu tarehe 14 hadi 18 Agosti, 2017 katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha International Conference
Centre jijini Arusha ambapo Tanzania imekabidhi nafasi hiyo kwa nchi ya
Burundi.
Nafasi ya uenyekiti ilikuwa
inashikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwakilishwa na Naibu
Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango Bw. Michael Muhoja nafasi ambayo
ameishikilia kwa muda wa mwaka mmoja. Katika kipindi hicho ameweza
kufanikisha utekelezaji wa majukumu yote 13 yaliyoanishwa kwenye mpango
kazi wa kamati hiyo ambayo inajumuisha wataalamu kutoka idara mbalimbali
za mamlaka za mapato kutoka Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Sudan
Kusini na wenyeji Tanzania.
Bw. Muhoja amekabidhi uenyekiti
kwa Bi. Martine Nibasumba kutoka Mamlaka ya Mapato ya Burundi ambapo
naye atatumikia kwa mwaka mmoja na atasimamia utekelezaji wa maazimio
ya kikao hiki ambayo yataidhinishwa na Makamishna Wakuu wa mamlaka za
mapato katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kikao hiki ni cha siku tano
mfululizo kitapokea ripoti kutoka kwa Wakuu wa Idara wa kila nchi
mshiriki kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali walizokubaliana
katika vikao vilivyopita na kupeana mrejesho wa hatua mbalimbali
walizofanya katika kuhakikisha kuwa shughuli za mamlaka za mapato katika
nchi za afrika mashariki zinatekelezwa kwa ajili ya maendeleo ya ukanda
mzima.
Akikabidhi ngao pamoja na nyundo
kama alama ya vifaa vya kutendea kazi ya uenyekiti, Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake Bw. Muhoja, amesema anakabidhi wadhifa wa
uenyekiti akiwa na amani kwa kuwa ametekeleza majukumu yake na
kuwashukuru wajumbe wote kwa kumpa ushirikiano mkubwa wakati wa
utekelezaji.
“Napenda kuwashukuru wajumbe wote
wa kamati ya ufundi kutoka nchi zote, na sasa nakabidhi rasmi nafasi ya
uenyekiti kwa mwenyekiti mpya kutoka Burundi,” amesema Bw. Muhoja.
Aidha, Bi. Martine, amepokea
nafasi hiyo ambayo inamfanya aongoze utekelezaji wa majukumu mbalimbali
kama yatakavyoainishwa na kamati pamoja kuidhinishwa na kikako cha
Makamishna Wakuu kwa ajili ya utekelezaji.
Katika Mkutano huu wa 80 nchi
zilizoweza kuhudhuria ni pamoja na wajumbe kutoka nchi za Uganda,
Rwanda, Burundi, Kenya na Tanzania, isipokuwa Sudan Kusini ambayo
hawakuhudhuria
No comments:
Post a Comment