Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel amevishauri
vyombo vya habari kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)
kujua lugha sahihi ya Kiswahili wakati wanapofikisha ujumbe wa kwa
jamii .
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es
Salaam wakati alipofanya ziara katika Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi
(MCL) ambapo ameeleza kuwa Baraza la Kiswahili lipo kwa ajili ya kukuza
na kuendeleza Lugha ya Kiswahili hivyo vyombo vya habari vina nafasi
kubwa katika matumizi sahihi ya Kiswahili.
“Vyombo vya habari mna nguvu kubwa
kwa jamii na mnafuatiliwa na watu wengi hivyo mnapaswa kujua matumizi
sahihi ya lugha ya Kiswahili katika uandishi,utangazaji pamoja na
matumizi mengine katika kuwasiliana na hadhira yenu,”alisema Prof.
Elisante.
Aidha, ameongeza kuwa ni wajibu
kwa wadau wa habari kusoma vizuri na kuelewa Sheria ya Huduma za Habari
na kutambua mambo muhimu yaliyoanishwa katika Sheria hiyo ikiwemo kuwa
na Mikataba,Bima ya Afya na Bodi na Mfuko wa Habari utakaowawezesha
kupata ufadhili wa kusoma.
Hata hivyo ameipongeza Kampuni ya
Mwanachi kwa kuwa na Kitengo cha lugha ya Kiswahili na maktaba nzuri ya
kuhifadhi magazeti yote ambayo yameshasomwa na kuvishauri vyombo vingine
kuwa na mfumo huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Francis Nanai amesema kuwa Kampuni yake
itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu yake kwa
manufaa ya nchi
No comments:
Post a Comment