Makamu wa Rais wa Itel Mobile
Bw.Leslie Ding akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya
Kampuni hiyo.
Balozi wa Itel Mobile,Irene Uwoya
akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.
………………………………
Kampuni ya Simu ya Itel Mobile
imetimiza madhamisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku ikiendelea
kufanya vizuri katika soko la mauzo ya Simu na kuwa kinara kwa ubora wa
bidhaa zake barani Afrika na nje ya Afrika.
Miaka 10 iliyopita Itel Mobile
ilizindua mpango wa kumwezesha kila mmoja kuwa na simu bora kwa ajili ya
mawasiliano ya uhakika,katika kipindi hicho chote tumepitia katika
kipindi kigumu katika Nyanja za kiuchumi na kisiasa lakini tumeweza
kufanikiwa kutimiza mlongo mmoja kwa uthabiti mkubwa.
Itel Mobile iliingia kwenye soko
la Afrika mwaka 2007 na baada ya kuanzishwa kwa timu ya watu wenye ujuzi
na moyo wa kufanya kazi na mpaka sasa miaka 10 kampuni hii imekuwa na
kuweza kuenea zaidi ya nchi 45 Duniani kote.
Ndani ya miaka 10 Itel Mobile
imekuwa na mabadiliko makubwa chanya ya bidhaa kutokana na kufuatwa
matakwa ya wateja wake hivyo imepelekea kupendwa na kuleta mvuto
kutokana na kuboreshwa kwa bidhaa hizo kwa ubunifu mkubwa.
”Tumeweza kuongeza idadi ya wateja
mara mbili zaidi barani Afrika na pia shukrani zetu za dhati ziende kwa
wateja wetu pamoja na mashabiki wote wa Itel na mpaka sasa tumeuza
jumla ya simu milioni 100’alisema Makamu Rais
Aidha nguvu kubwa yetu inatokana
na bidhaa zetu zilivyo bora pamoja na timu ya wafanyakazi wetu ambao
kila mmoja amekuwa akijituma kutokana na nafasi yake na pia ubora na
mvuto wa bidhaa unatokana na mapendekezo ya watumiaji wetu na huduma za
matengenezo baada ya mauzo na warantii ya miezi 12 kwa bidhaa zetu zote.
Hata hivyo tumekuwa na ushirikiano
na mastaa wa nchi za Afrikia kama mabalozi wa kampuni yetu na wamekuwa
kiungo muhimu katika kuleta ufahamu na uelewa kuhusu kampuni ya Itel
ambapo imekuwa kampuni 3 bora barani Afrika.
Na kwa kuonesha upendo wetu Afrika
tumekuwa tukifanya matendo ya ukarimu kwa jamii na kujitolea kutembelea
baadhi ya shule na vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kusaidia
wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.
Itel Mobile Tanzania kwa
kushirikiana na balozi wa kampuni mwaka huu peke mpaka sasa tumewasaidia
katika mahitaji muhimu zaidi ya watoto 400 wanaotoka mazingira magumu
wakiwemo yatima na tunaendelea kuunga mkono jitahidi za kusaidia jamii.
Tunaposherekea miaka 10
tunatarajia kuleta mabadiliko makubwa zaidi ili kuimarisha bara la
Afrika kwa kutoa bidhaa bora za mawasiliano na leo tunazindua simu mpya
ambazo ni za kisas zaidi yaani Itel S12 na S32 na zina ubora kutokana na
kuwa kila simu simu ina kamera mbili za mbele pia mwonekano mzuri na
kusaidia kuchukua selfie ya kundi ambayo ina uwezo wa kuchukua watu
wengi zaidi pia zina Fingerprint ‘alama za vidole’
No comments:
Post a Comment