• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 29 September 2017

    CRDB BENK WAONYESHA USHUJA MBELE YA RC MAKONDA



    Mkuu wa Mkoa  Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea  mifuko ya simenti elfu 10,000  kutoka benki  CRDB  kwa ajili ya ujenzi wa  Ofisi za Walimu .

    Baada ya ziara ya kukagua ghala la  kuifadhia vifaa vya ujenzi wa ofisi za walimu   leo katika eneo la Jeshi Mgulani ambapo  amekabidiwa mifuko ya Simenti 10,000kutoka benki ya CRDB 
    Paul  Makonda ameendelea kuishukuru CRDB Bank kwakuendelea kuunga mkono juhudi za ujenzi wa ofisi za Waalimu na kupitia dawati ambalo wamelianzisha la uchangiaji ujenzi huo anaimani kwamba utaleta tija kwa watanzania na hususani kwa wakazi wa Mkoa wa Dsm.

    "Tunatoa shukurani nyingi kwa Benki ya CRDB kwa kujitoa katika mchango wao wa milioni 100 ambapo fedha hiyo imetumika kununua mifuko ya cement" amesema.

    Aidha ameyataka  Makampuni  kuiga mfano wa benki hiyo kwani wakifanya hivyo kwa upande wa vifaa vya ujenzi haitokuwa shida na amewapongeza kwa kuwa pamoja na Serikali na kumuunga mkono Rais John Magufuli

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI