Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
“TIC nategemea mtakuwa na jukumu la kuziambia taasisi za zingine za serikali kwamba hamfanyi vizuri na kwamba mchezo wenu ni mauti kwetu, kama mimi natafuta wawekezaji nasafiri, nabembeleza, nasalimia watu ambao wasingepata nafasi ya kusalimiana na mimi, nakosa kukaa na familia yangu, nakosa kukaa kwenye jimbo langu, nasafiri nazunguka naleta wawekezaji halafu yupo mtu anatumia mwezi mzima au miaka miwili kutoa kibali, TIC mnapaswa mniambie” amesema Waziri Mwijage kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya TIC.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bwana Godfrey Simbeye ametahadharisha wanasiasa kuhusu kauli zao zinazowakatisha tamaa wawekezaji kuacha mara moja.
No comments:
Post a Comment