Katika
kuboresha huduma za kibenki nchini Maendeleo Bank lao imetoa zawadi kwa
washinidi wake wanne wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya ‘Maendeleo
pamoja na wewe’ iliyochezeshwa tarehe 31/8/2017 Jijini Dar es
salaamHafla ya kuwapatia washindi hao zawadi ilifanyika leo katika
ukumbbi wa ‘Mviringo hall’ uliopo makao makuu ya Benki hiyo ‘Luther
House’ posta Jijini hapa ambapo washindi hao wanne walijishindia zawadi
tofauti tofauti ikiwemo Ada za shule, tani za Saluji,Mabati pamoja na
kiwanja,
Akizungumza
katika hafla hiyo fupi mkuu wa kitengo cha biashara Maendeleo Bank
Peter Tarimo amesema katika kuhakikisha Maendeleo Bank inakuwa karibu na
wateja wao imeamua kuwahamasisha hasa wazazi kufungua Account za Benki
kwa ajili ya watoto wao ili kuweza kuwajengea utamaduni wa kuhifadhi
fedha
“Mtakumbuka
kuwa kampeni hii ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa nane na wateja
wengi walishiriki, Droo ilichezeshwa chini ya usimamizi wa bodi ya
michezo ya kubahatisha (Gaming Board) na kuwapata washindi hawa wanne
ambao leo tunakwenda kuwakabidhi zawadi zao”
Aidha
tarimo aliongeza kuwa Droo ya pili ya bahati na sibu hiyo inatarajiwa
kuchezeshwa mwezi wa Novemba mwaka huu na ya tatu itakuwa mwezi Disemba
ili kupisha zoezi la uuzaji wa Hisa litakaloanza tarehe 18/9/2017 na
kutarajiwa kumalizika mwezi October
Droo
ya pili ya mwezi Novemba itajumuisha wateja wapya waliofungua Account
katika Benki hiyo kuanzia kumalizika kwa Droo hii ya kwanza kwa
kuhakikisha kuwa katika Account zao kuna kiasi cha Shilingi Elfu Hamsini
na kuendelea
Washindi
walioshinda katika Droo hiyo ni Noela George Njavike alieshinda Ada ya
shule yenye thamani ya shilingi laki nne, mshindi wa Pili ni Simon
Anaufoo Urasa aliejishindia mabati, watatu ni Walter Moses Mchome
alieshinda Tani za Seruji na Mshindi wa Nne ni Sarah Fadhili Izumbe
aliejishindia zawadi ya kiwanja
Maendeleo
Bank Plc inatoa huduma za Benki zenye Gharama nafuu na rafiki kwa
wajasiliamali, wafanyabiashara , watumishi wa serikali na wananchi kwa
ujumla na kutoa wito kwa wateja wapya kwenda kufungua Akaunti Mpya





No comments:
Post a Comment