• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 21 September 2017

    Mganga Mkuu Igunga asimamishwa kazi kutokana na ubadhirifu wa fedha

    Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrer Mwanry ameagiza kusimamishwa kazi mganga mkuu wa wilaya ya Igunga Dr. Bonaventure Kalumbete ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha, zaidi ya Shilinigi million 23 na laki mbili pia ameagiza kukamatwa aliyekuwa kaimu mganga mkuu wilaya hiyo, Afisa ugavi,Mhasibu Idara ya Afya na Boharia wa Idara ya Afya ili wachukuliwe hatua za kisheria.

    Mwanri amefikia maamuzi hayo baada ya kubaini watumishi hao Godfrey Mgongo aliyekuwa kaimu mganga mkuu wilaya ya Igunga, Mohamed Mtao, Afisa Ugavi , Richard Byelembo Mhasibu Idara ya Afya na Jones Lotto Boharia idara ya afya waliagiza vifaa tiba kwa mzabuni Muhoro Traders lakini vifaa hivyo havikuwahi kupokelewa na halmashauri ya wilaya ya Igunga huku afisa Ugavi na Boharia wakikiri kupokea vivaa hivyo.

    Nao Viongozi wa wilaya ya Igunga wamewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani zama zimebadilika.

    Awali akiwa katika ziara yake wilayani Igunga Mkuu wa mkoa wa ametembelea baadhi ya vituo vya Afya na zahanati na kukuta baadhi ya akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakilalamika kutozwa pesa za matibabu kinyume cha utaratibu.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI