…………………
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina ameagiza kufungwa
kwa machimbo ya mchanga yaliyopo katika kijiji cha Kolangwa Wilaya ya
Mkuranga Mkoani Pwani kwa kile kinachodaiwa kusababisha uharibifu wa
mazingira na mali.
Mpina ametoa agizo hilo la
kufungwa kwa machimbo hayo alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa
mazingira mkoani Pwani mapema hii leo, ambapo amebaini uharibifu huo
umechangiwa na Taasisi za Serikali ikiwemo halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga, Idara ya Madini na Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira
NEMC, kwa kile alichokisema kuwa uchimbaji huo umefanyika bila wananchi
kushirikishwa na haukuzingatia miundombinu na sheria ya Mazingira pia
makazi ya watu.
.
Kufuatia mapungufu hayo, Mpina
ameagiza Taasisi hizo za Serikali kufuatilia uharibifu uliofanywa kwa
muda wa wiki mbili na kukaa pamoja na mfanyabiashara huyo anayemiliki
machimbo hayo kuona namna ya kuondoa kero hiyo inayowakumba wananchi pia
uchafuzi wa mazingira unaofanywa na machimbo hayo, hivyo amesema kama
kuna hasara yeyote ili mfanyabiashara huyo kulipa gharama hizo.
Awali Naibu Waziri Mpina
alitembelea kiwanda cha Azam kilichopo Mkuranga mkoani Pwani na
kuwapongeza kwa utunzaji wa Mazingira sambamba na hilo pia ameagiza
kiwanda hicho kupima Maji taka yanayozalishwa kiwandani hapo.
No comments:
Post a Comment