• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 27 September 2017

    Mwigulu aungana na wananchi


    Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Kinampanda ameanza ujenzi wa kituo kikubwa cha Afya katika kata hiyo.

    Waziri Mwigulu amesema ujenzi utaanza Oktoba 2 mwaka huu ambapo kwa kuanza yeye ametoa mifuko 300 ya Simenti na Nondo 100 huku akiwataka vijana wajitolee kufyatua matofali.

    Tayari mkandarasi wa ujenzi huo ameshapatikana na anaanza kazi Jumatatu ya Oktoba 2 ambapo matarajio mpaka ifikapo mwakani kituo hicho kianze kufanya kazi.

    Aidha kwa upande wa Vijana wa Iramba wakiwakilishwa na Katibu wa vijana CCM Abel Makala wamesema wapo tayari kuweka kambi sehemu kunapofanyika ujenzi huo mpaka ukamilike kuunga mkono juhudi za kupatikana kituo

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI