Mbali na eneo hilo la Manji lenye ukubwa wa ekari 715 eneo lingine ambalo rais ametangaza kufuta umiliki wake ni lenye ukubwa wa ekari 5400 lililopo Pemba Mnazi wilayani Kigamboni lililokuwa linamilikiwa na kampuni ya Amadori .
Rais Dk. Magufuli ameelekeza maeneo hayo sasa kuwa ni hifadhi ya ardhi ya serikali ambapo yatapingiwa matumizi mengine.
Hatua hiyo ya Rais, ilitangazwa Dar es Salaam, leo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati akihutubia mkutano uliohusisha watendaji wa juu wa Wizara, Mkoa wa Dar es Salaa na wilaya ya Kigamboni.
Waziri
Lukuvi amesema, rais ameridhia kufutwa kwa KDA na kuelekeza kazi zote
zilizokuwa zikifanywa na mamlaka hiyo sasa zitekelezwe na Halmashauri
ya Manispaa ya Kigamboni.
"Pia rais ameagiza wananchi wote walio katika maeneo yaliyopimwa kukabidhiwa hati zao na kuruhusu wananchi wilayani humo kuendeleza makazi na maeneo yao kuanzia sasa," alisema Waziri Lukuvi.
Aidha ametoa taarifa kwa wananchi wote juu ya shamba la AMADORI kuto fanya shughuli yeyote katika mpaka maelekezo yatakapo tolewa.
Na shamba ambalo lilikuwa likimilikiwa mfanyabiashara Yusufu Manji limechukuliwa na serikali mara baada yakushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 10.
Waziri Lukuvi ameeleza kuwa mamlaka ya KDA ifanye makabidhiano ndani ya miezi sita na nyaraka zote zipelekwe ofisi ya Mkurugenzi na watoe ushirikiano kwa Halmashauri ili waweze kushirikiana vyema na Halmashauri katika kuuendeleza mji wa Kigamboni.
Waziri Lukuvi ameeleza kuwa serikali itazidi kuchukua hatua kwa maeneo yasiyoendelezwa na kuwa mapori, huku akiwataka wenyeviti wa serikali za mitaa kuwa waangalizi na kufanikisha kuwa hakuna raia yeyote anayejenga Kigamboni bila kufuata taratibu.
Akizungumza baada ya maamuzi hayo ya Rais Mbunge wa jimbo la Kigamboni Faustine Ndugulile ameeleza sasa umefika wakati wa wanakigamboni kufurahia kuishi kigamboni na wataweza kukopesheka na kuuza maeneo yao, huku akiisisitiza mamlaka ya halmashauri kufanikisha kuwa mji huo unapangwa vyema na kuhakikisha unapimwa na hati zinatolewa kwa wakati.
"Tumeangaika sana tangu mwaka 2008 lakini tunatoa pongezi kwa Rais kwa kusikiliza kero yetu ya muda mrefu sasa wanakiga,boni wataweza kuuza maeneo yao na kukopesheka.




No comments:
Post a Comment