Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas
amefunguka na kusema kuwa hakuna masharti yoyote serikali imeweka ili
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu apatiwe matibabu na kusema
wanasubiri maombi ili waweze kugharamia matibabu ya Lissu.
Msemaji wa serikali amesema hayo jana
kupitia mtandao wake wa twitter siku moja baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA
Freeman Mbowe kusema kuwa alipata taarifa kutoka kwa wasaidizi wa Spika
wa Bunge kuwa wapo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu kwa
masharti ya kuwa mgonjwa lazima apelekwe India, wapate barua ya maombi
na kupata ripoti ya madaktari jambo ambalo Mbowe anasema alilikataa na
kusema hawezi kufanya hivyo.
Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo ndipo
Msemaji wa Serikali ameibuka na kusema kuwa hakuna masharti yoyote
ambayo wameyaweka na kusema serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya
Tundu Lissu na kuwa wao wanasubiri barua kujua gharama za matibabu.
"Hakuna sharti lolote, tunasisitiza tena
na bado tunasubiri, leteni barua rasmi tujue gharama na itifaki
nyingine za tiba. Tutagharamia" alisema Dkt. Abbas
No comments:
Post a Comment